David Kafulila: Serikali haipaswi kufanya Biashara. Biashara ni jukumu la Sekta Binafsi

David Kafulila: Serikali haipaswi kufanya Biashara. Biashara ni jukumu la Sekta Binafsi

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia (PPPC), Bwana David Kafulila, amesema sekta binafsi au ubia kati ya Serikali na sekta binafsi hujitokeza katika eneo ambalo kuna makutano ya maslahi kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.

Amesema kwa upande wa sekta binafsi, lengo kubwa ni kuongeza faida (profit maximization) kwa kuendesha shughuli zake kwa misingi ya biashara na uchumi.

Hata hivyo, si kila mradi una umuhimu kwa jamii unaweza kuendeshwa kwa misingi ya kibiashara, kwa sababu wakati mwingine idadi ya watumiaji au walipaji huwa ndogo kiasi kwamba mradi hauwezi kujilipa kibiashara.

Kwa hiyo, amesema eneo linalofanya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi uwezekane ni pale ambapo mradi unaweza kulipa kibiashara, lakini wakati huo huo Serikali inaona mradi huo kuwa muhimu kiuchumi au kwa maendeleo na ustawi wa wananchi.

Kafulila amesema katika mazingira hayo, Serikali inapaswa kuacha shughuli ambazo zina mvuto wa kibiashara zifanywe na sekta binafsi, ili Serikali iweze kuelekeza rasilimali zake kwenye maeneo mengine yenye umuhimu mkubwa kwa ustawi wa jamii ambayo sekta binafsi haiwezi kuyafanya kwa sababu hayana faida ya kutosha kibiashara.

Amesisitiza kuwa kwa kufanya hivyo, Serikali inaweza kutumia rasilimali zake kwa ufanisi zaidi, huku ikishirikisha sekta binafsi katika maeneo ambayo yanaweza kuendeshwa kibiashara na kuleta uwekezaji, ajira na maendeleo kwa wananchi.

Inashangaza sana kuona Bado Kuna watu wengi wajinga huko Halmashauri na idara za serikali,ona hiki 👇👇

View: https://www.instagram.com/reel/De349BdxqUF/?xtok=d2l5aGo5YmI5ajRn
 
Leo hii china mnayo isifia
Nusu ya makampuni nchini kwao
Yanamilikiwa na serikari yao
Halafu hapa Kuna wajinga wajinga
Wanasema haiwezekani.

Kama tunataka tuwe capitalist
Basi turuhusu Nguvu ya mtaji ndio iamue
Ardhi pia irudi mikononi mwa raia.
Sio hivi Sasa hata hatujielewi
Uelekeo na mustakabari tulio chukua
Serikali inamilik hisa Kwa ubia na sekta binafsi ambao ndio wanakuwa wenye sauti zaidi kwenye management
 
Back
Top Bottom