===
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini Tanzania (PPPC), Bwana David Kafulila, akijibu swali kutoka kwa Muhidini, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tengeru Institute of Community Development (TIDC), amesema kuwa jamii imara ni ile yenye stability na welfare.
“Tukisema tunataka kujenga Tanzania imara, cha kwanza ni stability. Iwe stable. Halafu cha pili ni welfare — iwe na ustawi. Jamii yenye amani na ustawi ndiyo jamii imara.”
Kafulila alieleza kuwa mchango wa serikali, civil society, vyombo vya habari, viongozi wa dini, NGOs na sekta binafsi ni muhimu katika kujenga jamii yenye amani na ustawi.
Fursa za Kila Mtu
Kafulila alisisitiza kuwa jamii imara ni ile ambayo kila mtu anaweza kufikia ndoto zake bila kujali background ya familia yake:
“Jamii imara ni ile ambayo mtoto akizaliwa maskini anaweza kufikia majaliwa yake bila kujali umasikini wa ndugu zake.”
Ameeleza kuwa Human Capital Index ya Tanzania na Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa sasa ni asilimia 40, lakini lengo ni kufikia 65–70% ifikapo mwaka 2050.
Maarifa Kama Sarafu ya Dunia
Kafulila alisisitiza kuwa maarifa ndiyo sarafu ya dunia:
Nchi zinapimwa kwa kiwango cha maarifa ya watu wake.
Uwezo wa watu wake huamua nani anakua namba moja duniani.
Sio wingi wa milima, dhahabu au mafuta, bali ni ubora wa watu.
Mageuzi ya Serikali na Sekta Binafsi
Akieleza historia ya mageuzi ya kiuchumi, Kafulila alisema:
“Tulikuwa na kipindi ambacho serikali inauza hata sukari. Serikali ikawa kubwa sana, na mzigo ukabebwa na mlipakodi. Wananchi wakasema no way — serikali kubwa sana lazima ipungue.”
Kwa mtazamo wake, mageuzi haya ni sehemu ya evolution ya binadamu na mabadiliko ya mifumo ya utawala kulingana na maendeleo ya jamii hasa kwa kutumia PPP.