Wanabodi, nimeikuta hii kwenye Tovuti ya kituo cha Ubia Kati ya Sekta binafsi na Sekta ya Umma PPPC imenivutia na ni mimi tu kuwaleteeni hii taarifa hapa.
Kafulila anasema ikiwa Taifa na Dunia tutaamua kuwashirikisha vema wanawake katika Ujenzi wa Uchumi wa Dunia au wa Taifa huenda Uchumi wa Dunia ukakua kwa 30% sawa na US$28 Trilioni.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa kituo cha Ubia nchini PPPC amerejelea utafiti uliofanywa na Kampuni ya Kitafiti ya McKinsey Global Institute iliyomtambua mwanamke kama turufu muhimu katika Ujenzi wa Uchumi Mkubwa wa Dunia.
Utafiti huu unapewa nguvu na uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan namna ambavyo kwa miaka minne tu Uchumi wa Tanzània umekuwa kwa record ambazo hatujawahi kuziona Wala kuzisikia tangu Uhuru wa Taifa hili.
==