Kila shujaa na wakati/vita yake. Ndio maana wengine wanaendelea kumuwaza Mwalimu Nyerere huku wakisahau kuwa yeye aliishi maisha yake na akafanya aliyostahili kufanya hivyo hivyo kwa Mzee Mwaibula.
Tunachojifunza hapa ni kuwa wanaozaliwa sasa hivi tu watu tusiotumia akili, wanyonge na dhaifu na ndio maana tunayaona yote haya. Swali la kujiuliza ni: huu ujasiri wa kukatiza ruti watu wa daldala wanaupata wapi na wewe unyonge wa kutowakatalia au kudai chako umeurithi kwa nani!?
Mkuu,Kipindi cha mwaibula watumiaji wa usafiri wauma (daladala)tulipata nafuu/uhakika wa usafiri wa daladala kwani daladala zilikuwa hazikatishi ruti gari ilivyo andikwa ndo inapoenda kuanzia mwanzo wa kituo hadi mwisho kama ni Gongolamboto-mwenge inakuwa hivyo hivyo nowdays daladala zinakatisha ruti kwa makusudi bila kuchukuliwa hatua yoyote.Mfano jana mapema kabisa saa 7 nimepanda daladala ya bugurun mbezi nimepanda wametucharge bugurun ubungo sh400 kufika ubungo 2kashushwa hapo hapo wakatangaza mbez 2kapanda ruti ya mia 500 tukatozwa sh800.jamani mwaibula na vijana wako tunaomba mrudi maskini Dar 2nanyanyaswa/tunabanwa kila kona.
Kumbukumbu nzuri sana!
Mchango wa huyu Ndugu ni mkubwa kweli hasa kwa abiria tunaotumia usafiri wa daladala kwenda hapa na pale.
Utaratibu ulioanzishwa chini yake wa daladala kuandikwa njia unatusaidia sana hivi sasa na kutupunguzia gharama. Sipati picha ningekuwa natumia kiasi gani kwa siku kutoka na kurudi Kimara ninapojibanza. Sasa hivi hata konda akiitia mwisho Ubungo napanda tu ili mradi ni Kimara
Sijui yuko wapi, lakini mchango wake binafsi ninauthamini sana. Mwenyezi amjalie popote alipo Mheshimiwa sana David Mwaibula
Mzee mwaibula yupo, nilionana nae mwezi uliopita kwenye kitafrija flani. ....yupo sinza, ukifika uwanja wa tp kuna kanisa la wasabato, ukiuliza hata mtoto naenda kwa mwaibula basi unapelekwa