David Mwaibula, aliyebuni mistari ya daladala Dar es salaam yupo wapi?

David Mwaibula, aliyebuni mistari ya daladala Dar es salaam yupo wapi?

Huyu mtu yuko wapi? Alileta rangi ya daladala, alileta njia za daladala, alileta sare na heshima kwa abiria. Anastahili tuzo.
 
Serikali imemtupa kabisa,huyu kwa kweli alikua jasiri mwenye ubunifu.Ilifaa awe mkurugenzi DART
 
Hakukaa ofisini. Aliwafuata wenye daladala walipo. Hakujua wakati ule watu hawakupenda mabadiliko.
 
Tatizo Lake Alikua Anafanya Kazi Nje Ya Mfumo.
 
Tatizo bado Makondakta wengi hawako smart ata madereva wa daladala zile sare zao hawazijali ata kuzifanyia usafi na kuzipiga pasi achalia mbali utunzaji wake utakuta wana azimana huyu anatoka zamu anamvulia shati mwenzie.
 
Lile benzi lake likionekana tu sehemu wakatisha ruti wote wanapotea barabarani.
 
Yupo bado ana nguvu za kufanya kazi.Nilimuona kwenye kikao.
 
Tatizo Lake Alikua Anafanya Kazi Nje Ya Mfumo.
Nje ya Mfumo? Kivipi? najua watu waliotaka kumtoa ndiyo walikuja na wazo la Sumatra halafu yeye akachwa hana cha kufanya. Leo na enzi za Mwaibula na kama mtoa hoja anavyosema "Mzee wa Pama" alikuwa ni mbunifu sana na alikuwa angalau anapambana kuweka mfumo wa usafiri Dar es salaam uwe wa maana. Nafikiri alipoingia kwenye siasa akagombana na wakubwa wakampoteza!
 
Wanajamvi mambo vipi? David Mwaibula aliwahi kuwa mkurugenzi wa SUMATRA na alivuma sana lakini alipotea ghafla. Siku hizi yuko wapi?

Hali kadhalika, Ezekiel Malongo alikuwa mahiri sana TBC. Nae yuko wapi siku hizi? Mwenye habari please tiririka. 🙂
 
kuhusu Mwaibula waulize makonda wa zamani hasa walokuwa wakikatisha route.

ezekiel malongo beki mstarabu wa kupanda na kushuka, kwa habari zilizokuwepo ni kuwa.............................. mara ya mwisho inasemekana alikuwa mlevi sana,(pombe zetu).
 
Ezekiel Malongo alishatangulia mbele za haki nadhani mwaka jana.
 
Ndugu wanajamvi nimejiwazia kwa sauti ningemwomba Rais wetu Mh Magufuli aturejeshee Ndg Mwaibula kwenye kile kitengo chake alichokuwa zamani angalau hata kwa mwaka mmoja tu ili aweze kuleta ile ari na ubunifu kama aliokuwa nao mwanzo si makosa kumrejesha,

Kama alivyorejeshwa Ndg Philip Mangula ndani ya nafasi za juu CCM ili kukiimarisha chama vya kale dhahabu kila kukicha kwenye usafiri kwa wanaokaa pembezoni ya mji afadhali ya jana nawasilisha.
 
Naona unampigia chapuo, huna maslahi binafsi kweli.
Pili; Ungekuja na hoja inayoshawishi na siyo kulinganisha mambo ya serikali na ya chama
 
Nchi Ya Viwanda Hii Huyo Hata Sasa Hawezi Kubali
Unadhani Yeye Alishaweka Heshma Yake Ila Akirudi Inaweza Kushuka
 
Hapana,sinza e alishapewa heshima yake kuna sehemu panaitwa kwa mwaibula.kuhusu ubunifu wacha vitakuja vichwa vipya vitafanya mazuri.
 
Back
Top Bottom