David Mwaibula, aliyebuni mistari ya daladala Dar es salaam yupo wapi?

David Mwaibula, aliyebuni mistari ya daladala Dar es salaam yupo wapi?

Kuna hii tabia ya makondakta na madereva kukatisha safari ,hawafiki mwisho wa safari husasan katika Jiji la dar es salaam.

Jana nilipanda daladala ya kutoka mbagala kwenda muhimbili.nilivyoingia ndani nikamsikia Mzee Moja,miaka yake kama
Yule askari wa Mataa namba yake uliipata wapi? Maana hakuna maelezo kama ulichukua ila maelezo yako tu ulimpigia.
 
Abiria wa mbagala ni wajinga sana nimeishi huko najua adha yake, Yan konda atawatenda anavyotaka hawasemi kitu.

Kuna Ile daladala za kariakoo ikifika saa nane haziji sehemu watu wanapandia siku zote, zinakaa kula nyuma Ili watu wapande Kwa nauli ya mzunguko.

Ukihoji kwanini natozwa nauli zaidi abiria ndio watakujibu umetaka siti ukae lipa nauli ulioambiwa ni kero sana
 
Jana nilipanda daladala ya kutoka mbagala kwenda muhimbili.nilivyoingia ndani nikamsikia Mzee Moja,miaka yake kama zaidi ya 60 hivi,analalamika kwa nini konda amechukua ela ya abiria alafu anasema hafiki muhimbili
Ila hiyo route mmmh!!
 
Kwani hujuiagi kama huyu ni Trafik?

Huyo mwamba sikuwa namjua mkuu kwani ningemtegemea pia kumsikia kwenye hii ya kuvuana manguo:

IMG_20230311_090130.jpg


Uzi wa mjumbe huu hapa:

Kosa La Mtu Kupakilia Abiria Sehemu Isiyo Na Kituo Adhabu Yake Ni Nini.

CC: Midazolam
 
Unauzalendo kamanda kweli kweli ila sisi wengine tutakuvunja mwoyo, mimi naonaga ma konda wengi ni wehu sina mda wao na wachiaga Mungu, na hiyo nauli ya 400 naiona kama Sadaqa
Hizi ndio akili za kitanzania.
 
nafasi yako ndoimekubeba oelse ungenyanyasika tu kama sisi abiria wengine hii nchi usipokua unamjua mtu mkubwa au wewe kuwa na wadhifa flani utanyanyasika tu
Tatizo abiria sisi ni waoga na wajinga.
Ndio maana makonda kwa kulijua hilo wanafanya hivyo.
Watu wako wawili vs nyie mko zaidi ya kumi mnashindwaje kutetea haki yenu.
Ni ukondoo tuu.
 
Bongo Hapo Zamani:

Mwaibula Alikuwa Mbabe Wa Jiji...

- Mwanzilishi wa mifumo kwenye route za Daladala

Ndugu zangu,

Kila Jiji duniani lina wababe wake.

Na ubabe wa maana ni ule ubabe wa kusimamia taratibu.

Enzi hizo David Mwaibula alikuwa ni mmoja wa wababe wa Dar es salaam kwenye kusimamia taratibu. Nimewahi kukutana na kuongea naye mara kadhaa kwenye moja ya vijiwe vya jijini Dar.

Hakika, jamaa alikuwa ni msimamizi mkuu na mahiri wa masuala ya Daladala jijini. Huyu alikuwa haswa ' Mzee wa Daladala'.

Mbali ya mabadiliko mengine, ndiye aliyeasisi utaratibu wa madereva na makondakta wa Daladala kuvaa sare.

Na jamaa alikuwa mbabe haswa. Akimkuta kondakta amevaa kandambili alimshusha na kumwambia arudi nyumbani akafuate viatu vyake.

Maana, kwa Mwaibula, mtu lazima uheshimu kazi yako. Huwezi kwenda kazini na kandambili.

Mwaibula alibuni ruti mpya nyingi za Daladala. Ndiye aliyeanzisha pia utaratibu wa Daladala kuwa na mikanda ya rangi kuonyesha ni ya route gani, aidha, kuandika mbele kwa rangi na maandishi makubwa kama ni Temeke - Posta au Kariakoo. Maana, makonda walikuwa na tabia ya kubadilisha vibao vya ruti zao.

Hakika, nchi kwa ujumla inahitaji kuwa na idadi fulani ya ' Wababe' wenye ujasiri wa kuanzisha mambo mapya na wenye kuhakikisha taratibu zinafuatwa.

Na hapo nchi hiyo lazima itasonga mbele kimaendeleo.

Yapata mwezi hivi nilikuwa kwenye moja ya mgahawa, Morogoro Mjini. Mara akaingia Mwaibula na pama lake kichwani. Tukakaa kunywa chai na kuongeha mwanzoni kabisa alichoonyesha kukerwa nacho ni uona Mji wa Morogoro kutokuw na usafiri wa Daladala wenye kueleweka. Ni vurugu tu, kama alivyosema.

Mwaibula ndiye pekee mjini aliyekuwa akiendesha Benzi iliyotumika Ikulu ya Nyerere.
Aliwezaje kununua Benzi chakavu ya Ikulu?

Ni Tafakuri Jadidi.
 
Back
Top Bottom