Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Chama cha Kijamii (CCK) kupitia mgombea wa chama hicho, David Mwaijojele, wakati wa uzinduzi wa kampeni kitaifa wa chama hicho zilizofanyika viwanja vya kwa Tesha, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo, kimesema endapo kitapewa ridhaa ya kuongoza dola kitaenda kukomesha mikopo kausha damu na kuja na ya kuongeza damu.
Mwaijojele amesema wanafanya hivyo kutokana na mikopo kausha damu imekuwa tatizo kubwa kwa wananchi na kuwasababishia umasikini,ambapo watu wamekuwa wakinyang'anywa mali zao zikiwemo thamani za ndani pamoja na kuuzwa kwa nyumba zao.
"Niwahikishie mkituchagua CCK tunaenda kukomesha yote haya,badala yake tutakuja na mikopo ongeza damu ambapo sasa mtu ataweza kununua thamani za nyumba, kununua kiwanja na hata kujenga nyumba kwa sababu Serikali ya CCM imeyashindwa kuyafanya yote haya," amesema mgombea huyo.