David Nkuba a.k.a Mac D hatunaye tena.

David Nkuba a.k.a Mac D hatunaye tena.

Polen wanafamilia kw Msiba,lakini ingekuwa vizuri kwa anayemfahamu kuweka hata kipande kidogo cha mistari ya wimbo wake mmoja ili watu wamtambue kwa hapa bado inachanganywa wanamzik wenye majina kama hilo wako wengi.
 
Nyie mnaomjua vizuri tuambieni basi aliimba wimbo gani maana wengine hata hatumkumbuki.,anyway RIP broda
 
Mungu Mwenyezi katika Jina la Yesu aliyemuumba David Nkuba hatimaye amemrudisha kwake.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa na Jina la Bwana libarikiwe. Amen (Ayubu 1:21).
Poleni sana wafiwa, Mungu Mwenye enzi katika Jina lipitalo majina yote Jina la Yesu Kristo awafariji wakati huu mgumu. Amen.
 
Mac Dee yupi, aloimba na Dully Sykes ule wimbo wa jimama?
 
R.i.p broda.. Lakn mleta mada amekurupuka, hana habari kamili za kumuhusisha marehemu na muziki.. Au na ye amesikia tu alikuwa mwanamuzk, ndo mana kashndwa kujbu maswali.
 
ameacha album ngapi? huyu ndo yule wa dar skendo au?
R.I.P Kamanda.
 
Kila nafsi itaonja mauti, mola awape faraja mke, mtoto, pamoja na familia yote ktk kipindi hiki cha majonzi.
 
R.I.P Mc Dee!

Tunaomba picha yake apa jamvini!
 
Mleta Taarifa, habari yako bado inapwaya wadau wanataka kujuwa huyu ni Mac D yupi? kwa sababu Mac D ninayemjuwa mimi Mama yake ana Bar pale maeneo ya Airport na kama sikosei hawa ni vijana wa Airport pamoja na Soggy Dogy, Suma G na kundi lao la Hotpot Family, tungeomba uijazie nyama hii Taarifa yako.
 
Sikujua kama Nkuba alikuwa mwanamuziki. Kama anayedhaniwa kuwa amefariki ni yule mwanamuziki aliyekuwa chini ya P-Funk,basi huyu ninayemzungumzia siye. Kwa maelezo ya mwanzisha uzi,nina uhakika marehemu siyo Mac Dee aliyekuwa chini ya P-Funk. Labda kama alikuwa mwanamuziki kwa jina lingine;ndiyo maana nimeanza kwa kusema "sikujua kama Nkuba alikuwa mwanamuziki".
Ninasema hivyo kwa kuwa mke wake ni ndugu yangu kwa mbali.

Ni kweli amefariki,lakini siyo leo,amefariki jana pamoja na mjomba wake mmoja. Walikuwa wakienda Kahama,Shinyanga kupeleka gari jipya (lilitoka kununuliwa Dar) la mjomba wake mmoja aliyekuwa akiumwa Dar.

Inasemekana mjomba aliyekuwa akiumwa ndiye aliyekuwa akiendesha gari,nafikiri ni maeneo ya Singida ama Manyoni ndiyo walipopata ajali baada ya tairi kupasuka. Nkuba na mjomba wake 1 ndiyo waliofariki (alikuwa na wajomba 2 katika safari). Mjomba aliyekuwa akiumwa,hajafariki.

Msiba upo pale UDSM,Ubungo Flats,eneo linaitwa Geti Maji. Ni geti la kuingilia UDSM kwa kutokea Ubungo. Mipango ya awali inasema marehemu Nkuba anaweza kuzikwa Kahama. Ingawa kwao kabisa ni Kahama. Kuna mtafuruku kidogo wa kindugu.

Bwana alitoa,bwana ametwaa. Jina lake lihidimiwe.

Pumzika kwa amani kaka Nkuba.
 
''Mac Dizo, Pfunky prodakshizo'' alikuwa akipenda kutamka maneno hayo kwenye nyimbo zake.
 
Back
Top Bottom