David Opati Etale azungumzia uanajeshi wake Uingereza

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
September 2017
Nairobi, Kenya

David Opati Etale azungumzia uanajeshi wake Uingereza : Dira ya wiki
Mchezaji mpira wa kandanda nchini Kenya kwa jina David Opati Etale baada ya kuona mpira wa kulipwa haulipi Kenya akaamua kuacha soka na kujiunga jeshi la Uingereza. Alichezea timu kubwa za kandanda Kenya kama Tusker FC, Kenya Commercial Bank n.k

Alijunga Jeshi hilo la Uingereza akiwa na umri wa miaka 21 baada ya kuomba nafasi ya uaskari kupitia intaneti na kukubaliwa kwa vile Kenya ni nchi mojawapo ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth). Baada ya mafunzo ya awali ya miezi sita ktk Jeshi La Uingereza huko ulaya alipelekwa nchi za Iraq na Afghanistan kutumikia jeshi la Uingereza.
Source: KTN news Kenya
Bahati Mbaya wakati akiwa huko Afghanistan gari lao la deraya lilikanyaga bomu la kutega ardhini na kupata kilema cha kupoteza mguu mmoja hospitalini Uingereza. Kabla ya kupoteza mguu wake, juhudi kubwa zilifanywa katika hospitali za Uingereza kwa kufanyiwa operesheni 8 mpaka 12 kujaribu kuokoa mguu wake lakini madaktari baadaye walimwambia inabidi mguu ukatwe kuokoa maisha yake.

Kwa Hivi sasa David Opati Etale anafanya kazi ya kuwapa matumaini wale wote waliopitia changamoto zinazowafanya kukata tama ya maisha. Maana David Opati Etale baada ya kuona mengi katika uwanja wa vita nchini Iraq na Afghanistan na pia kupoteza mguu wake mmoja alikata tamaa ya maisha akataka kujidhuru PTSD (Post-Traumatic Stress Disorder in Military veterans).

Pia anafanya kampeni ya uelewa nchini Kenya wa jinsi ya kuwahudumia askari wote wenye matatizo ya afya ya ubongo (PTSD) baada ya kukabiliana na mambo ya kuogofya walipokuwa uwanja wa vita kama Somalia na Sudan ya Kusini.

Matatizo ya kukata tamaa ya maisha huwapata pia vijana wa kizazi kipya kutokana na mitandao ya kijamii kupitia intaneti na hivyo David Opati Etale anasisitiza vijana wapatiwe sapoti wanapoonyesha dalili za kukata tamaa ya kuishi.
 
Sept 2017
Nairobi, Kenya

INSPIRATIONAL THURSDAY: David Etale Part 1
Etale, ex-British soldier narrates ordeal in Afghanistan war that led him to loose his leg.
He talks about how he joined the British army. The Training and eventually his deployment to Afghanistan.
[HASHTAG]#JeffAndJalasOnHot96[/HASHTAG]
Source: Hot 96 FM Kenya
 
INSPIRATIONAL THURSDAY: David Etale Part 2

Source: Hot 96 FM Kenya
 
I lost my leg in Afghanistan, almost gave up
Meet David Etale, a Kenyan-born UK veteran soldier who abandoned his football career to join and fight for the UK military. Etale was deployed to Afghanistan, a war zone whose aftermath made him attempt taking his life away twice.
Source: Tuko / Tuco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…