David Raya | Joan García | Unai Simón — Nani anastahili kuwa kipa namba 1 wa Uhispania?

David Raya | Joan García | Unai Simón — Nani anastahili kuwa kipa namba 1 wa Uhispania?

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Mjadala huu umekuwa mkubwa hasa kutokana na viwango walivyoonesha makipa wote.

Je, kocha wa Uhispania aendelee kumuamini Unai Simón ambaye amekuwa chaguo la kwanza kwenye mechi zote za kufuzu Kombe la Dunia, au awape nafasi David Raya na Joan García ambao wamekuwa katika kiwango bora sana kwenye klabu zao?

Simón ana faida ya uzoefu na kuaminika kwenye timu ya taifa, lakini Raya amekuwa nguzo muhimu kwa Arsenal kuchukua kombe la ligi na kucheza fainali ya Klabu bingwa Ulaya, huku Joan García naye aking'ara akiwa sehemu ya kikosi cha Barcelona kilichochukua Ubingwa wa ligi

Swali linabaki: timu ya taifa inapaswa kuongozwa na kipa mwenye uzoefu mkubwa wa kimataifa au yule aliye katika kiwango bora zaidi kwa sasa?

Wewe ungemchagua nani kuanza golini kwa Uhispania, na kwa nini?

Spain.jpg
 
De Gea akiwa wa moto kwenye ligi alipoitwa timu ya taifa alitoa maboko balaa.
 
Ana footwork mbovu sana sio sweeper mzuri kwa uchezaji wa Spain mashambulizi yanaanzia chini kwa kipa (build up) hawezi kutoboa.

Hapa namba ni ya Unai Simon.
Iker Casilas, De Gea
Wote walikuwa na weakness hiyo
Ila binafsi naamini Kwa Sasa Raya ni goal keeper namba 1 duniani
 
Back
Top Bottom