David Silinde: Ili kuwakomesha Zambia kwa kutufungia mpaka, Serikali yetu iwaongezee Tozo kwenye mizigo yao iliyopo bandarini Dsm

David Silinde: Ili kuwakomesha Zambia kwa kutufungia mpaka, Serikali yetu iwaongezee Tozo kwenye mizigo yao iliyopo bandarini Dsm

Silinde ni mbumbumbu kilaza ni mbunge juha kabsa hana anachojua zaidi ya unafiki

Lakini pia nafikiri tatizo lipo ndani ya CDM ilikuwaje kuwaje mpaka wakafikia kupitisha jina la mtu kama huyo na wenzake ambao sasa karibu na Bunge kuisha ndio wameanza kuonyesha utovu wa nidhamu, nafikiri mechanism yao ya kupitisha majina inabidi ifanyiwe marekebisho makubwa na waache kukimbilia uwingi wa viti bungeni
 
Kwani wao kufunga mpaka ni kuwakomoa watanzania au ni kuwalinda wananchi wao na maambukizi ya corona.Tanznaia wananchi hawadhaminiwi na hata wenyewe hatujidhamini hata kidogo .Viongozi wa nchi yetu ni kutaka watu wafanye kazi tuuuuu mnakufa shauri zenu ,mnaumwa mtajaza wenyewe ,mkifa mtaenda kutupwa huko sijui UNONIO kama takataka usiku.Tunachojua ni kodi kodi ,kwani inawacost what kuongea kukubaliana na kushirikiana na wenzetu basi tutume timu yetu ya madaktari na wahudumu wa afya wakashirikiane pale mpakana wawapime wawa karanteen nk.Sasa sisi tumekuwa na viburi kama vile dunia yote ya kwetu na tunaweza tukawatawala hata majirani.Mkifanyiwa hivyo na nchi zenye ukwasi mnawaita mabeberu yaani hamweleweki.Mgekuwa nguvu inayotumika kuwatafuta,kuwanyanyasa CDM na kidogo wapinzani tunatumia kufanya vitu vya maendeleo tungekuwa mbali sana aiseee.
 
Kesha hamia ccm jumba la Mashudu naona kesha anza kushusha mzigo
 
Silinde analeta za maamuzi ya "ukichaa kichaa" ule ambao Mafichoni King anaupenda. Hapo anatumaini Mafichoni King anamuona na anaweza kumkumbuka hata uDC iwapo atashindwa kurudi Bungeni. Ila asisahau huyo Mafichoni King anaweza akaishia muhula 1.
Membe January Nape Kitwanga lugola na wenzao wengi wanataka mtukufu aishie hapo waweke mtu mwingine warejeshe Serikali toka Dodoma kurudi kule Dsm, hawataki kuona mtukufu na Naibu Rais Daud Bashite wanarejea madarakani tena
 
Sikujua kuwa jamaa ni sifuri kiasi hicho bora wamefurusha akawe Mbunge wa Spika kuliko kuwa na mtu wa hivyo
Mmmh!! Mkuu Silinde siyo sifuri, yaani mnasahau haraka mno, yule prof. wa jalalani kwani alikuwa hivyo? Slow Slow naye alikuwa hivi alivyo sasa? Yaani hapo Sillinde bado kabisa, ndiyo kwanza gari hata halijawaka,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani wao kufunga mpaka ni kuwakomoa watanzania au ni kuwalinda wananchi wao na maambukizi ya corona.Tanznaia wananchi hawadhaminiwi na hata wenyewe hatujidhamini hata kidogo .Viongozi wa nchi yetu ni kutaka watu wafanye kazi tuuuuu mnakufa shauri zenu ,mnaumwa mtajaza wenyewe ,mkifa mtaenda kutupwa huko sijui UNONIO kama takataka usiku.Tunachojua ni kodi kodi ,kwani inawacost what kuongea kukubaliana na kushirikiana na wenzetu basi tutume timu yetu ya madaktari na wahudumu wa afya wakashirikiane pale mpakana wawapime wawa karanteen nk.Sasa sisi tumekuwa na viburi kama vile dunia yote ya kwetu na tunaweza tukawatawala hata majirani.Mkifanyiwa hivyo na nchi zenye ukwasi mnawaita mabeberu yaani hamweleweki.Mgekuwa nguvu inayotumika kuwatafuta,kuwanyanyasa CDM na kidogo wapinzani tunatumia kufanya vitu vya maendeleo tungekuwa mbali sana aiseee.
Nguvu inayotumika kuudhofisha chadema ingekuwa imetumika kupambana na corona leo hii kusingekuwa na kifo hata kimoja na mjadala huu usingekuwepo kwa mataifa Jiran wangekuwa na imani na Afya za watanzania wote
 
Hivi chadema Kuna Nini? Yani kitendo chakufutwa uanachama tu Kila kitu kinapotea hapohapo dah!!
 
Huyu dogo Silinde amechanganyiwa sasa, nilikuwa upande wake ila naona amepotoka vibaya sana.

Silinde kumbuka bila mpaka wa Zambia pengine wewe usingekuwa mbunge 2010 Jimbo la Tunduma.

Ni fedha za wananchi wa Tunduma zilizotokana na mpaka wa Zambia ndio zilikupatia wewe ubunge, Ile jeuri ya kukuchangia hela ya kampeni, hela ya kula, hela ya mavazi na kila kitu ilitokana na mpaka huu.

Leo unasema serikali iengeze tozo kwenye mizigo ya Wazambia, njoo Tunduma uangalie ndani ya hizi siku tatu uone maisha wanayoishi Wanatunduma.

Hakuna kabisa mzunguko wa hela, hakuna kwacha, hakuna kiazi Wala mchele unaovuka huko....hakuna Nguo Wala vifaa vya ujenzi vinavyovuka huko Ile jeuri ya Wanatunduma imekata kabisa....

Nenda pale Kisimani uone kama watu wameshika hela kama siku zote ..piga simu kwa watu wako waulize nini kinaendelea Tunduma.

Serikali inaathirika ila wananchi wa kawaida ndio tunaathirika zaidi.

Watu kila siku wanaamka asubuhi wanasikiliza serikali ya Zambia itasema nini kuhusu huu mpaka..hakuna tamko lolote zaidi ya gari za Askari zinazozurura kulinda mpaka.

Hivi umejiuliza kuhusu Watanzania waliotapakaa Ndani ya Zambia nzima kuanzia Lusaka,Ndola,Kitwe kote huko Watanzania hawahesabiki...Unataka na wao wapewe masharti magumu ya kuishi huko.?

Umejiuliza Watanzania wenye maduka upande wa Zambia hapa Tunduma maarufu kama eneo la black...mpaka leo mamia ya maduka ya Watanzania yamefungwa na soko lote umejiuliza kuhusu familia zao wanakula nini wanaishije na familia zao.?

Leo Zambia imeruhusu maduka ya vyakula kufunguliwa lakini maduka ya Watanzania hawajaruhusiwa Wala kuvuka hawajaruhusiwa.

Unaongea kama huijui Tunduma kweli wewe Silinde unaetaka kurudi Tunduma kuchukua jimbo unatoa kauli hiyo kweli..

Nakushauri hiyo kauli tolea huko huko bungeni ukija kusemea hapa Tunduma utapigwa mawe mchana kweupe hata usiamini kinachoendela...

Bado WanaTunduma wanaimani na wewe ila kwa kaulizi hizi watakususa mapema sana na hutaamini.

Tena ikibidi waombe radhi Wana Tunduma, hiyo kauli ingetolewa na wabunge wengine tusingeshangaa maana wengi hawajui hali halisi ya Tunduma.ile sio wewe.

Ulietoka Dar na nauli tu kila kitu kuhusu maisha yako kikaanzia Tunduma.

Tunachosubiri WanaTunduma na Watanzania kwa ujumla ni mikakati ya pamoja kati Tanzania na Zambia ili shughuli ziendelee kama kawaida.

Kilichopo sasa ni kwamba serikali ya Zambia haina imani kabisa na Mtanzania yoyote yule kila wanaemwona wanahisi ana Corona.

Jaribu kuwa kiongozi mwenye maono, nchi zetu hizi maskini tunategemeana sana hatuwezi kukomoana ana akapatikana mshindi...

Ulisema unataka kukua kisiasa ila sasa naona unashuka viwango kwa kasi badala ya kupanda....
Dungai anawadanganya hawa, sasa ili aonekane anafanana nao ameharibu kabisa, ndo basi tena hiyo kashapotea
 
silinde hongera kwa kupigania wapiga kura wako ambao biashara zao zimefungwa maduka yao upande wa zambia hawawezi kwenda.Jimbo lake linapakana na Zambia ambako maelfu ya wafanyabiashara wa Tanzania hawawezi fanya biashara zambia ambako ndio tegemeo lake kubwa

Silinde haongelei tu hewani anaongelea wapiga kura wa jimbo lake la Momba

KOsa la pili chadema wanafanya kumzomea mbunge asiongelee maslahi ya wapiga kura wake wanaoumia kwa mpaka wa zambia kufungwa
Wadau. Eti Huyu ndo think tank wa ccm
 
Wadau. Eti Huyu ndo think tank wa ccm
Na wewe ndio think tank ya chadema uliyeshauri wabunge wafukuzwe kwenye chama eti wamekosea kuhudhuria vikao vya bunge wakati kazi ya mbunge ni kuhudhuria vikao ivi una akili timamu wewe?
 
Back
Top Bottom