David Silinde: Serikali inajenga 'vyumba vya ubaridi' Rungwe kupunguza upotevu wa zao la Parachichi baada ya kuvunwa

David Silinde: Serikali inajenga 'vyumba vya ubaridi' Rungwe kupunguza upotevu wa zao la Parachichi baada ya kuvunwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Njombe, Rebecca Msemwa, amehoji Serikali kuhusu changamoto wanazokumbana nazo wakulima wa maparachichi katika mkoa huo.

Anaeleza kuwa kuwa licha ya Njombe kuwa maarufu kwa uzalishaji wa maparachichi bora, mkoa huo hauna vyumba vya ubaridi (cold rooms) kwa ajili ya kuhifadhia mazao hayo, jambo linalosababisha maparachichi kuharibika kwa haraka baada ya kuvunwa.

Kutokana na hali hiyo, anaiomba serikali kueleza ni lini itawatafutia wakulima hao masoko ya uhakika ili waweze kunufaika na kilimo hicho.

Pia, unaweza kusoma hoja ya Mdau ~ Serikali ilitushawishi tuwekeze katika kilimo cha Parachichi, sasa imetutelekeza, Madalali wanatuharibia soko

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde anafafanua kuwa serikali inatambua mchango wa zao la parachichi na imekuwa ikichukua hatua mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kugawa miche ya ruzuku kwa wananchi.

Kuhusu miundombinu ya uhifadhi, anaeleza kuwa kwa sasa serikali inajenga vyumba vya ubaridi katika maeneo ya Rungwe kupitia mradi wa TFSRP, na mkoa wa Njombe pia umejumuishwa katika mpango huo wa kujenga miundombinu ya ubaridi ili kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvunwa (post-harvest losses).

Aidha, anaongeza kuwa serikali inaendelea kuwahamasisha wawekezaji kwenda kuwekeza mkoani Njombe ili kuhakikisha kunakuwepo na soko la uhakika la maparachichi.
 
Cold room moja ndogo hata 10M haifiki, Yani hata wakichangisha kijijini wanaipata.

Huu uzwazwa wa kijamaa wa kutegemea serikali kwenye kila kitu umetufikisha pabaya mno
 
Cold room moja ndogo hata 10M haifiki, Yani hata wakichangisha kijijini wanaipata.

Huu uzwazwa wa kijamaa wa kutegemea serikali kwenye kila kitu umetufikisha pabaya mno

Kwa kipato gani walichonacho?

Kodi zao zinaenda wapi? Acheni kuchukua kodi zao wajenge kila kitu wao wenyewe.
 
Back
Top Bottom