David Silinde: Wabunge acheni kutumia hela za mfuko wa jimbo kununulia samani zenu

David Silinde: Wabunge acheni kutumia hela za mfuko wa jimbo kununulia samani zenu

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
7,207
Reaction score
17,674
Dodoma. Serikali imeeleza kuwa fedha za mfuko wa majimbo zipo kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya wananchi na sio za kununulia samani za ofisi za wabunge.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu Mei 23, 2022 bungeni na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), David Silinde ambaye amesema kuwa fedha hizo za mfuko zipo mahususi kwa ajili ya kuchochea maendeleo kwa wananchi.

Silinde alikuwa anajibu swali la Mbunge wa Lulindi (CCM), Issa Mchungahela ambaye ameuliza ikiwa Fedha za Mfuko wa Jimbo zinaweza kutumika kununulia samani za ofisi ya jimbo.

Mchungahela ameuliza kama jibu ni hapana, samani katika ofisi za wabunge zinapaswa kununuliwa na nani ili wabunge wawe na ofisi zenye hadhi ya kibunge.

Naibu Waziri amesema mfuko wa kuchochea maendeleo ya Jimbo ulianzishwa kwa Sheria Na.16 ya mwaka 2009 na kwamba fedha za mfuko wa Jimbo ni mahususi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kijamii iliyoanzishwa na wananchi wa jimbo husika.


“Mheshimiwa Spika, halmashauri zilielekezwa kuwapatia wabunge ofisi kwa ajili ya shughuli zao ikiwa ni pamoja na thamani kulinganaa na uwezo wao wa ukusanyaji mapato yao ya ndani,” amesema Silinde.

Naibu Waziri huyo ameagiza wakurugenzi wa halmashauri kushirikiana na wabunge katika kutekeleza majukumu yao ili kuondoa malalamiko na kufanya maboresho ya ofisi hizo.
 
Mibunge ya CCM hovyo sana, pesa imeambiwa ni za mfuko wa jimbo yao yanalazimisha yajinunulie 'mazagazaga' na kuhonga 'vimada' wao.
Screenshot_20220430-141754.png
 
Back
Top Bottom