Wakati wa maonesho ya FIFA Countdown Concert yaliyofanyika jijini Los Angeles, msanii maarufu wa Nigeria Davido alivutia hisia za wengi baada ya kuvaa koti maalum lililobeba majina ya wanafunzi 39 pamoja na walimu saba waliotekwa nyara kutoka Halmashauri ya Oriire (Oriire LGA) katika Jimbo la Oyo, nchini Nigeria.
Hatua hiyo imeelezwa na wengi kuwa ni ishara ya kuwakumbuka waathirika hao pamoja na kuendeleza uhamasishaji kuhusu umuhimu wa usalama wa watoto na walimu, hasa katika maeneo yanayokumbwa na changamoto za kiusalama.
Kupitia jukwaa hilo kubwa la kimataifa, Davido alitumia nafasi yake si tu kuburudisha mashabiki, bali pia kupeleka ujumbe mzito wa kijamii unaogusa maisha ya watu wengi barani Afrika na duniani kwa ujumla.
Kitendo hicho kimepokelewa kwa hisia tofauti na wengi wakimsifu kwa kutumia umaarufu wake kuzungumzia masuala nyeti yanayohitaji umakini wa jamii na mamlaka husika. Swipe kuona zaidi na utoe maoni yako.