Nigeria inao wasanii wangapi? Wangapi wamezungumzia utekaji na ugumu wa maisha? Msanii mmoja Davido mmemgeuza ni tasnia nzima ya burudani ya Nigeria imezungumzia utekaji.
Msanii sio msemaji wako na sio muwakilishi wako popote chini ya jua, na hakuna utaratibu wowote unambana awe msemaji wako. Msanii ni Mfanyabiashara wa burudani kama wafanyabiashara wengine na sio jukumu lake kukusemea wewe, akiamua kusema kama alivyofanya Davido ni hiari na wala sio lazima.
Mtu mmoja asiye na akili atakwambia sisi ndo tunawafanya wasanii wapate pesa, sisi ni wateja wa Pepsi tunanunua bidhaa zao, wanaingiza pesa kupitia sisi, Mbona hatuwashurutishi waongelee utekaji? We si ni mteja wa Voda? Mbona huwashurutishi waongelee shida zako? We si ni mteja wa Coca? Mbona huwashurutishi waongelee shida zako? Kwanini msanii? Au kwasababu unaona unammudu?
Usisubiri msanii akusemee, paza sauti yako, kama hutaki kupaza sauti subiri Gigymoney atakusemea🤣🤣🤣