Davido hana furaha na label yake ya Sony

Davido hana furaha na label yake ya Sony

Hizi labels kubwa hazijui soko la muziki Africa. Kuna mifano lukuki ya wasanii kupotea mara tu waliojiunga na hizi labels; Rose Muhando, Mayunga, Nakaaya Sumari, D'banj na sasa Davido. Wasanii wajifunze kitu tatizo wakiambiwa wanadhani wewe ni hater
 
Mwenzetu anayerokodiwaga video sauzi naona alotema big g akakubali Katanga za kuonjeshwa
 
Tatizo mahaba yakizidi ni shida nakumbuka uzi ulikua na facts za kutosha ila watu walipinga haya sasa yameanza kutokea[emoji41]
Kabisa mkuu ule uzi naukumbuka vyema jamaa aliandika vizuri sana na alieleza vizuri sana lakin team bush man waliponda vikali kiukwel nilitaka niulize hivi huyu davido nowadays simsikii kuna ni.
Mkuu uliyeleta ule uzi wa sony big up aisee ngoja uone watakavyotafuta mchawi
 
Hizi labels kubwa hazijui soko la muziki Africa. Kuna mifano lukuki ya wasanii kupotea mara tu waliojiunga na hizi labels; Rose Muhando, Mayunga, Nakaaya Sumari, D'banj na sasa Davido. Wasanii wajifunze kitu tatizo wakiambiwa wanadhani wewe ni hater
Ivi kumbe Mayunga nae alijiunga nao?
 
Sasa yule ndugu yangu wa mtaa wa kariakoo kitongoji cha mabondeni jangwani
sijuo itakuaje kuaje sababu uezo wake wa kifedha tu no shida

MTU kama davido ambae pesa kwake sio za kutafuta zipo kwao mkwanja mrefu wanamsumbua kutokana na mikataba yajabuhajabu
Sasa king kiba wa kariako sitakua shida
 
Ivi kumbe Mayunga nae alijiunga nao?
Mayunga alikua universal studios aliunganishwa direct aliposhinda lile shindano ila sasa hayupo nao alivunja kandarasi.
 
Mayunga alikua universal studios aliunganishwa direct aliposhinda lile shindano ila sasa hayupo nao alivunja kandarasi.
Wewe unahisi kosa la Mayunga ni lipi? Au wewe ungekuwa ndio Mayunga Ungechukua uamuzi gani mbali na aliouchukua Mayunga?
 
Yule wa kwetu yeye anamaajabu 7 au 21?? Na hao sonny
 
Kabisa mkuu ule uzi naukumbuka vyema jamaa aliandika vizuri sana na alieleza vizuri sana lakin team bush man waliponda vikali kiukwel nilitaka niulize hivi huyu davido nowadays simsikii kuna ni.
Mkuu uliyeleta ule uzi wa sony big up aisee ngoja uone watakavyotafuta mchawi

Alisema hivi yule mdau

Huko kwenye mitandao ya kijamii kumechafuka habari ya Ali kusign deal na Sony wengi wakiamini huo ndio utakuwa mwanya wa msanii huyo kutoboa kimataifa.. Jambo ambalo mashabiki wake wanashindwa kuelewa ni kuwa huo unaweza kuwa anguko la King Kiba badala ya kuwa neema..

Kwanza kabisa kitu ambacho hawakielewi ni kuwa Ali hajasaini na Sony Music Ent. BMG (ishu yake sio 'global deal') bali amesaini na Sony Music Africa ambayo ni subsidiary ya Sony Music Entertainment!! Kwa ninavyoelewa Sony Music Africa wana sambaza mziki na kumanage wanamuziki ndani ya Africa pekee.. Sasa eidha Ali hajui alichosaini au chumvi inaongezwa kunogesha habari..

Kingine watu wanaona hii ni kama Bahati Ali amepata wanachoshindwa kuelewa ni kwamba wasanii wakubwa Africa huwa wanakataa kusign na hizi kampuni zenye asili ya marekani na ulaya kutokana na kampuni hizi kushindwa kutimiza malengo na kutoelewa mazingira ya soko la mziki Africa! Kwa mfano wasanii wote ambao wamewahi kusign na Sony karibia wote walikuja kufa kimuziki kutokana na Sony kushindwa kuwa market kutokana na kutoelewa mziki wa Africa; mfano wasanii kama Nakaaya Sumari, Nneke Egbuna (Nigeria), Luncvile (SA), Nathan Ro (SA) wote hawa wamepotea kwenye mziki..

Mfano mwingine ni msanii D'banj ambaye aliondoka Mavins na kujiunga na label ya GodLife chini ya kanye west, mpaka sasa D'banj anasafiria jina lake tu lakini kimuziki ameshuka vibaya sana!! Kampuni za kimarekani hazina record ya kuwatoa wasanii wa kiafrika na hii inatokana na kutoelewa industry yetu na ndio maana Psquare walikataa mabilioni waliyotaka kupewa ili wasign Convict records..

Kingine kinachosemwa na watu ni kwamba hizi kampuni zina mambo mengine makubwa zaidi kwahiyo inakuwa nguvu kwao kuwa serious sana na mwanamuziki mmoja mmoja; kwa mfano kampuni mama ya Sony Music Africa (Sony Entertainment BMG) ina zaidi ya label 25 ndogo ndogo kama hii aliyosign kiba na ina wasanii karibia katika kila nnchi ya ulaya, Asia na Amerika ya kusini. Wana zaidi ya wasanii elfu moja wanaowasimamia so inakuwa ngumu kwao kutoa macho kwa msanii mmoja mmoja na ndio maana wasanii wengi wakubwa wa Africa wanakataa kusign chini yao wanaona ni afadhali watengeneze timu zao wenyewe za management ambazo macho yao na attention yote itakuwa kwao wao kama wasanii..

Anyways, let me just assume management ya Ali inafahamu vitu ambavyo mimi sivifahamu na wamefanya research ya kutosha kabla ya kusign na hatimaye watatuprove wrong wote ambao tuko sceptical about this deal.!!
Kama kijana mwenzangu namtakia kilala kheri na mafanikio katika safari yake mpya...
 
Ni miezi 9 sasa tangu asaini mkataba na Sony Music lakini Davido hajatoa wimbo mpya.
Mashabiki wamechoka kusubiri, yeye mwenyewe amepagawa na mambo yamekuwa si mambo tena!

Kulikuwa na mipango ya kuachia kazi mpya Ijumaa hii, September 9, lakini imeahirishwa tena na staa huyo uvumilivu umemshinda.

Tetesi kutoka Nigeria zinadai kuwa Davido hana furaha tena na uongozi wa label yake. Na sasa ameamua kuonesha masikitiko yake kwenye snapchat yake

Chanzo: Bongo5
bado baraka na kiba
 
Wewe unahisi kosa la Mayunga ni lipi? Au wewe ungekuwa ndio Mayunga Ungechukua uamuzi gani mbali na aliouchukua Mayunga?
Ningevunja mkataba kama alivyofanya Mayunga. Kuna video YouTube Mayunga akihojiwa na bongo5 kuhusu mizengwe aliyopitia akiwa under US unaweza icheck ukipata nafasi. Hizi labels hazijui kabisa soko la muziki Africa bora Dayamondi na wengine waliokataa kuingia huko
 
Nilitaka kusema kwamba Mayunga yeye hana kosa alilofanya kuanzia mwanzo mpaka mwisho cuz aliwatumia sonny badala sonny kumtumia mayunga, then akawamwaga
 
Back
Top Bottom