Nigeria imepiga marufuku nyimbo kadhaa kuoneshwa kwenye TV na kupigwa katika vituo vya redio.
Agizo hilo limetolewa na tume ya udhibiti wa matangazo, Nigeria Broadcasting Commission.
NBC imesema- kupitia barua kwenda kwa vyombo vya habari kuwa nyimbo zilizopigwa marufuku zina "picha chafu, na kuonesha maisha ya majivuno na kifahari".
Baadhi ya nyimbo zilizoathirika na hatua hii ni pamoja na wimbo wa Wizkid- In My Bed, Fans mi wa Davido, Shakiti Bobo wa Olamide na Inyanya, na Don Jazzy na wimbo Gift.
Hawa hawana tofauti na BASATA huu wimbo wa olamide shakiti Bobo sijaona wapi kuna picha chafu.