Davido, Wiz kid, Olamide na Iyanya wafungiwa

Davido, Wiz kid, Olamide na Iyanya wafungiwa

kedrick

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2015
Posts
5,080
Reaction score
4,914
Nigeria imepiga marufuku nyimbo kadhaa kuoneshwa kwenye TV na kupigwa katika vituo vya redio.

Agizo hilo limetolewa na tume ya udhibiti wa matangazo, Nigeria Broadcasting Commission.

NBC imesema- kupitia barua kwenda kwa vyombo vya habari kuwa nyimbo zilizopigwa marufuku zina "picha chafu, na kuonesha maisha ya majivuno na kifahari".

Baadhi ya nyimbo zilizoathirika na hatua hii ni pamoja na wimbo wa Wizkid- In My Bed, Fans mi wa Davido, Shakiti Bobo wa Olamide na Inyanya, na Don Jazzy na wimbo Gift.

Hawa hawana tofauti na BASATA huu wimbo wa olamide shakiti Bobo sijaona wapi kuna picha chafu.
 
Kumbe na huko wana BASATA yao eeh ka nyimbo ni mbovu zifungiwe tu hamna namna
 
Dah kuna ile moja ya phyno inaitwa yayo aisee ni balaa !! Kuna mzigo mmoja iviiii balaa sanaaa
 
Safi sana mtu anaposhindwa kufata sheria anatakiwa kunyooshwa kabisa..Hongera NBC!

Pia kwa hapa tanzania naendelea kuwapa pongezi BASATA kwa kumfungia Shilole na kama mnasoma hapa naomba muongeze muda ikiwezekana iwe miaka 2!
 
Dah kuna ile moja ya phyno inaitwa yayo aisee ni balaa !! Kuna mzigo mmoja iviiii balaa sanaaa

Haaah iyo video hatari demu lina ji tingisha phyno Ana kuambia yayoo oba go nayo pia imepigwa ban
 
Safi sana mtu anaposhindwa kufata sheria anatakiwa kunyooshwa kabisa..Hongera NBC!

Pia kwa hapa tanzania naendelea kuwapa pongezi BASATA kwa kumfungia Shilole na kama mnasoma hapa naomba muongeze muda ikiwezekana iwe miaka 2!

Miaka miwili shishi byb c atakuwa kashachukua waume wa watu n kuvunja ndoa za watu wengi sana
 
Back
Top Bottom