Shetani yupo na ana nguvu pia kwa wasioenda kwa mataka ya mwenyezi Mungu, kwa maana hiyo wapo wanaotumia hiyo mittishamba kwa kuwashika waume za watu na kuwafanya kama mandondocha yao, na ukifanyiwa hivi wanasema sio rahisi kujijua ni watu wanaokuzunguka ndio watakujua, wewe utajiona upo poa sana.
Pia mume akitoka nje na kupata hawara sio lazima awe amelishwa limbwata wengine ni mambo tu ya mahaba yamewachanganya kwa hao mahawara wao. unajua mahawara wanakuwa hawana majukumu mengi kama wake muda mwingi wanakaa wakitafuta mbinu za kuwaridhisha wanaume wao, huku home mke anakuwa na majukumu kibao, watoto labda wanne wamefatana, anafuga kuku, anafanya kazi anapika kwa ajili ya familia, akilala anakuwa mchovu, hapa mume akitoka na demu yuko single, anaishi mwenyewe, nyumba muda wote ipo neat, mazingira yale yanamlewesha mume anashinda hukohuko, akirudi home ni kulala. Kw hiyo bwana mkubwa unaweza pewa limbwata likakukolea na unaweza usipewe ukapagawa tu mambo ya mahaba unayofanyiwa na kimwana wa pembeni