Dawa gani ni nzuri ya kuhifadhia maharage

Sasa hivi kila sehemu duniani wanajaribu kutokutumia kabisa kemikali kwenye mazao. Nchi zilizoendelea ukiingia supermarket unakuta kuna bidhaa za kilimo zenye lebo ya ''organic'' kuonyesha kuwa mazao hayo hayakuwekwa kemikali. Na bei yake ni kubwa zaidi. Tanzania tukitaka bidhaa zetu ziwe na soko zuri itatubidi tuanze kilimo kisichotumia kemikali.
👏👏👏👏👏👏🙏🙏🙏🙏🙏
 
Nunua diaba zile kubwa kabisa,unayaweka na kufunga kwa mfuniko wake for good measure unaweza kuyatia dawa kwani wakati unayaweka yanaweza kuwa tayari wadudu waliingia,ila Kama una hakika yako salama,ukiyaseal yanakaa miaka bila kuharibika
Aiseeee bonge moja la ubunifu
 
Wadau kama kichwa cha habari kinavojieleza, nina kama gunia 30. Naomba mwenye kujua dawa nzuri ya kuhifazia maharage anijuze kwani nahitaji kuyaweka kama miezi minne..

Najua wajuvi mnaodili ni hili zao mpo.

Natanguliza shukrani kwenu
Nimesoma Maua Seminari na tulikuwa tunalima mahindi na baada ya kuvuna tulikuwa tunahifadhi kwenye mapipa safi bila ya kutumia dawa yoyote. Maua Seminari tulikuwa tunachukua 'Mchepuo wa Kilimo'. Hivyo, tulikuwa tuna'practice' kanuni za kilimo bora na utunzaji bora wa mazao ya chakula bila kutumia kemikali za viwandani. Tulikuwa tunajifunza pia kanuni za ufugaji bora wa wanyama na kuku, upandaji miti, grafting, uzalishaji wa mayai, utotoaji wa mayai, artificial insemination etc. Kwa upande wa usafishaji wa mapipa, tulikuwa tukichemsha maji hadi kufikia 100 za Celsius na kisha kuyaweka kwenye pipa moja baada ya lingine kwa lengo la kusafisha liwe safi na lisiwe na mafuta. Then, tulikuwa tunaweka pia mchanga safi na kuliviringisha ili maji na mchanga yafike eneo lote la ndani na kisha tukishajiridhisha kuwa limekuwa safi, tuliliacha likauke na baada ya kukauka tulikuwa tunapeleka mapipa safi stoo iliyokuwa na mapipa mengi kuanzia chini hadi juu na kwa mapipa ya chini tulikuwa tunalaza mbao kadhaa side by side ili tuweze kupanga safu nyingine ya mapipa hadi juu kabisa kwenye dari. Kama sikosei stoo yetu ilikuwa na uwezo wa kuchukua mapipa kama 100 hivi. Wakati wa kuvuna mahindi na baada ya kuondoa magunzi na kubakiza punje za mahindi, kazi iliyofuata ni kujaza mahindi yaliyokauka vizuri kwenye mapipa tupu na tulifanya hivyo hadi yale ya juu na kisha kufunga kwa mifuniko yake. Yalikuwa yanakaa hata zaidi ya mwaka mmoja na yalikuwa hayaharibiwi na wadudu. Pia mdogo wangu aliwahi kuvuna mahindi na kuniomba nimnunulie dawa ya kuhifadhia mahindi na nilimshauri asitumie dawa, bali kama ana mapipa atumie mapipa na kama hana nilimshauri anunue ndoo zinazouzwa baada ya kutoa mafuta ya kula na afanye kama nilivyoeleza hapo juu. Naye alinipa mrejesho kuwa nilimsaidia sana kupata njia nzuri ya kuhifadhi mahindi bila kutumia dawa na hata yeye mahindi yake yalikaa muda mrefu bila kuharibika. Nakushauri hata wewe tumia njia ya aina hii. Utaipenda na kuwasaidia wengine wanaotafuta namna bora ya kuhifadhi nafaka, ikiwa ni pamoja na maharage. Jaribu.
 
Naona watu mnazungumzia majaba na mapipa ila sasa kwa mwenye gunia 100 ananunua majba mangapi?bei ya jaba/pipa moja ni sh ngapi??? Tuanzie hapo.
 
Ahsante sn kaka
 
Halafu nilitaka kutoa angalizo kuwa ;
Yale mapipa mnayosema yanafaa mimi naona kuna changamoto ya kuwa:

Huwa ni used,

Hayajatengezwa kwa makusudi ya kutunza nafaka la hasha.

Mengi yametumika katika kuhifadhi kemikali mbali mbali ambazo hutumika kama malighafi za viwandani.

Je hizo kemikali hamuoni ni hatari pale unapobana pipa kiasi cha kufanya hewa isipite?

Je chakula kutunzwa kwenye pipa la kemikali ni salama kiafya?

Tafakarini
 
Well said
 
Back
Top Bottom