Dawa ipi itafaa kukaushia kidonda cha Opresheni?

Dawa ipi itafaa kukaushia kidonda cha Opresheni?

Peace92

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2013
Posts
261
Reaction score
57
Habari wana jamvi, mimi ni mama nimejifungua kwa upasuaji jumatatu ya tarehe 5 mwezi huu wa 5. Baada ya upasuaj niliruhusiwa kurudi nyumbani lakni naona kidonda kinatoa majimaji upande wa kulia pamoja na damu kidogo.

Juzi na jana nilirudi hospital wakanisafisha tu na leo hali ni ile ile, ndugu zangu nauliza je kuna dawa ya kufanya majimaji au kidonda kikauke haraka?

Asanten jaman nipo mikoa ya nyanda za kusini.
 
Unatumia dawa gani antibiotic uliopewa hospitali.?
 
Mimi nakushauri ni bora uanze sindano mara moja

Ceftriaxone for injection USP (powercef 1g) ni sindano 5 kila siku moja

Ni dawa moja nzuri sana na inakausha kwa haraka
Ukishachoma mbili we mwenyewe utaona mabadiliko...
 
Pole sana mamie pia hongera,jitahidi kidonda kisipate joto,mm nilipona ndani ya wiki,nilikiacha wazi kwa muda mrefu,na ukishaoga paka asali yako,tulia,utaona matokeo
 
Inspector: inategemea na umbile la mama yawezekana ni mnene so ana mafuta mengi mazoezi ni tiba nzuri pia na aina ya upasuaji aliofanyiwa kama ni ya mlalo na ye ni mnene basi lazima itafunikwa na tumbo kidonda kinakuwaje wazi??
 
Last edited by a moderator:
Ngoja nikupe uzoefu mkewe aliwahi fanyiwa upasuaji wa tumbo alikuwa na kidonda kikubwa sana alikuwa ana safishwa kwa uso halafu anapakwa Asali afunikwa na gouze anafungwa na plasta alipona dressing ilikuwa ya kila siku
 
Peace92 njoo uwaambie madaktari umbile lako na ujumuike kuwaeleza jinsi operation ilivyofanyika ili upate msaada mzuri na utakao kufaa.
 
Peace92 njoo uwaambie madaktari umbile lako na ujumuike kuwaeleza jinsi operation ilivyofanyika ili upate msaada mzuri na utakao kufaa.

Mim ni mwembamba sana na nimepasuliwa mlalo. Nilipewa dawa aina ya gluxalini nimemaliza lakini kidonda kimekauka upande mmoja tu na mpaka Leo cjatolewa nyuzi
 
Inspector: inategemea na umbile la mama yawezekana ni mnene so ana mafuta mengi mazoezi ni tiba nzuri pia na aina ya upasuaji aliofanyiwa kama ni ya mlalo na ye ni mnene basi lazima itafunikwa na tumbo kidonda kinakuwaje wazi??

Mim ni mwembamba na kidonda wamenishauri nikifunike kila cku nipo sehemu za baridi huku
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mamie pia hongera,jitahidi kidonda kisipate joto,mm nilipona ndani ya wiki,nilikiacha wazi kwa muda mrefu,na ukishaoga paka asali yako,tulia,utaona matokeo

Mim wamenikataza kabisa kuoga ulwezaje kuoga jaman? Je asali nipake ktk kidonda au?
 
Nimekushauri hapo juu mi mwenyewe nilifanyiwa operataion..katika paja langu baada ya kupigwa risasi na majambazi..

Kodonda kilikuwa kidogo baada week kikatanuka madaktar wakaamua nitumie hiyo sindano hapo juu fatilia comment yangu

Nilipopiga sindano ya pili nikaona mabadaliko kidonda kikaanza kufunika..ni sindano tano tuu kila siku moja ni nzuri sana hiyo dawa..ndio antibiotic ya mwisho kwa mujib wa Daktari wangu..

Kiukweli sindano hiyo usichome matakoni choma kwenye mshipa ni dawa kali sana fanya hivyo asee

Nakushauri pia kabla hujapaka chochote nenda kwa Doktor kwanza.. na usikifunike na bandeji kiache wazi
Na usikimwagie maji na mimi nilifanya makosa kama hayo.. kwa kujidanganya et nakisafisha..
 
Ukishaanza sindano rudi hapa kuleta feedback kwa faida ya wengine
 
Pole dear mimi mwenzio nilipasuliwa mlalo mwezi wa pili na ni mnene haswa mshono ulikuwa unafunikwa ila nilipona ndani ya wiki tu kuna cndano nilichomwa siku tatu nikapewa na vidonge vya wiki tu na mazoezi nilianza siku ya pili baada ya operation nakuomba jikaze inauma ila ndo ivo
 
Back
Top Bottom