Naomba ushuhuda wa mtu aliyekuwa na bawasiri ya ndani akatumia dawa iwe ya hospitali au Tiba mbadala akapona atusaidie na sisi maana tumetumia hizo dawa za kienyeji mpk tumechoka Hela tu inaenda na km ni dawa ya dukani atutajie maana wanadai bawasiri pia inapunguza zile nguvu.
Naomba kuwasilisha
Habari!
Binafsi ningependa kujua kama hiki unachotibu ni bawasiri/haemorrhoid.
Ombi ni kufika kwa mtaalamu wa afya kuthibitishwa na kupata mwelekeo wa kiasi cha tatizo kwani sijaona ni kwa jinsi gani umefikia kulielewa tatizo. Si kila njia aliyotumia mwenzako huwa pia inafaa kwako kwa tatizo lolote la kiafya. Hii inatokana na maelezo hapa chini.
Tunahitaji kuwa waangalifu tunapo tafuta tiba, suala linaloonekana dogo laweza kuwa kubwa au kutatuliwa kirahisi kulingana na njia utakayochagua kupita.
Wakati mwingine tumejikuta wenye msongo wa mawazo kwa kuona unatumia tiba sahihi lakini haupati nafuu. Kumbe hauko kwenye utaratibu unaofaa.
Mfano:
Bawasiri ni matokeo ya presha kwenye mishipa ya damu/veini kwenye eneo la haja kubwa.
Kuna aina mbalimbali ya visababishi, vyote vikihusishwa na mwongezeko wa msukumo kwenye njia ya haya kubwa:
*choo kigumu(yapo mengi hapa kwenye mwenendo wa maisha: kuto kunywa maji ya kutosha, kutokula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama matunda, mboga za majani, ulaji wa nafaka kamili.
*ujauzito(kwa akina mama).
*kunyanyua vitu vizito.
*asili: kuta za njia ya haja kubwa si imara sana na kwa jinsi tunavyo simama ni rahisi kuachia kutokana na kolamu ya damu ndani ya mishipa husika.
Nk.
Bawasiri hutokea kwa kufuata sehemu ilipo mishipa husika. Kwa kufuata mfumo wa saa, saa 12, 03, 12 na 09. Unaweza kupata eneo moja au zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Pia huweza kujirudia eneo la zamani kama visababishi havikufanyiwa kazi.
Kuna aina ya bawasiri kulingana na sehemu:
- internal/ ya ndani
- externa/ya nje
Pia kuna grade za haemorrhoid:
1: grade ya kwanza: yenye dalili, mfano maumivu au kutoa damu lakini haichomozi.
2: grade ya pili: Inayochomoza na kurudi baada ya kujisaidia.
3: grade ya tatu: Inayochomoza na kurudi kwa jitihada/kurudishwa.
4: grade ya nne: Inayochomoza na hairudi.
Hata kwa jitihada binafsi.
Pia kuna acute/ndani ua muda mfupi na chronic/iliyokaa kwa muda mrefu.
Richa ya aina, grade na muda husika(acute/chronic) pia kuna suala la complications/ matatizo ambatanishi mfano: kuwa na mpasuko/fissure, embolism/ kuziba kwa njia husika ya damu, maambukizi/infection kwa eneo husika.
Ili tiba iwe kamilifu ni vyema mtoa huduma na mpewa huduma kuzingatia haya yote.
Hapa ndo uchaguzi wa:
1: Aina ya tiba(kutumia dawa vs upasuaji).
Aina ya dawa vs aina ya upasuaji.
2: tiba mwambata, ili kurahisisha uponaji na kuondoa visababishi vya tatizo kurudia.
NB: Kwa njia yoyote unayoamua kupata tiba, husisha wataalamu wa afya ili uweze kujua ni kitu gani na cha kiasi gani unachofanyia kazi.