Dawa/njia gani inatibu vipele vya ndevu vinavyosababishwa na kunyoa?

SUBMAC

Member
Joined
Apr 12, 2024
Posts
11
Reaction score
11
Habarini wanajamvi!

Naombeni msaada wa njia ama dawa inayoponya vipele vinavyotokana na kunyoa ndevu. Nimejaribu kubadili njia mbadala za kunyoa, kama vile mashine, magic, wembe nk, lakini hakuna iliyoniletea nafuu.

Tafadhali nishaurini!
 
Kabla yakunyoa ndevu Fanya maandalizi chemsha maji yawe ya moto kiasi, chukua taulo safi kisha loweka kwenye hayo maji yakiwa Yana motomoto kisha kamua na weka kwenye kidevu huku ukikikanda. Kikianza kupoa (taulo) kifunge eneo la kidevu kisha kitoe. Unaweza kunyoa ndevu ( tumia sharp blades) bàada ya kumaliza tumia aftershaves (kama hauna tumia maji ya limao kupaka kwenye eneo ulilonyoa). Then 💥 you are ok.
 
Maji ya moto mithili ya yale ya kunyonyolea kuku
 
Kabla yakunyoa ndevu Fanya maandalizi chemsha maji yawe ya moto kiasi, chukua taulo safi kisha loweka kwenye hayo maji yakiwa Yana motomoto kisha kamua na weka kwenye kidevu huku ukikikanda. Kikianza kupoa (taulo) kifunge eneo la kidevu kisha kitoe. Unaweza kunyoa ndevu ( tumia sharp blades) bàada ya kumaliza tumia aftershaves (kama hauna tumia maji ya limao kupaka kwenye eneo ulilonyoa). Then 💥 you are ok.

Dr, hii ni kwa mwenye shida ya ingrown hair!?
 
Habarini wanajamvi!

Naombeni msaada wa njia ama dawa inayoponya vipele vinavyotokana na kunyoa ndevu. Nimejaribu kubadili njia mbadala za kunyoa, kama vile mashine, magic, wembe nk, lakini hakuna iliyoniletea nafuu.

Tafadhali nishaurini!
Tumia Grace Shampoo paka kwenye eneo unalotaka kunyoa then nyoa ukimaliza nawa zako maji ya kawaida tu. vipele utavisikia kwenye bomba
 
Paka limao siku 7 baada ya kunyoa .. usiku kabla ya kulala paka then unapolala nawa uso wako vizuri utaona vipele vinavyopukutika. Mm kwa sababu ya usomi wangu nilidharau mambo ya limao. Nikanunua mavipodozi ya pesa nyingi na wala hayakunisaidia. Nilipona kwa limao la 200 tu[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kingine usipende kushare mashine za kunyolea. Nunua ya kwako. Kuna magonjwa ya ngozi yanakujaga kwa kushare hizi mashine coz huku mitaani hawajui vizuri namna ya kusterilize zile mashine kabla ya kumnyolea mtu mwingine
 
Unanyoa kila baada ya muda gani? Na ndevu zikianza kuota unasikia muwasho eneo hilo?
 
Tumia maji ya moto au Vuguvugu baada ya kunyoa, Tumia Tube, Tripple action De creme hutajuta
 
Pia unaweza kupata dawa ya kuchua iko kwenye kichupa inaitwa RoBB hii haina mpinzani
 
Back
Top Bottom