Lamchina
JF-Expert Member
- Nov 12, 2010
- 240
- 120
KITUNGUU maji ni kiungo kinachotumika hasa jikoni na wengi wamekuwa wakijua hivyo.
Lakini kiungo hiki kikifika kinapohitajika kwa ajili ya tiba jina lake ubadilika na kuitwa Allium Cepa.
Kitunguu maji kama kilivyo kitunguu swaumu ni viungo vya ajabu ambavyo vimeshatoa majibu katika tiba, na hasa pale linapokuja suala la ugonjwa wa kisukari.
Ndani ya kitunguu maji kunasadikika kuwepo tiba muhimu iitwayo kitaalamu kama Allyl Propyl Disulphide (APDS) na Diallyl Disulphide Oxide (Allicin) na mchanganyiko wa falconoids ambazo hutibu maradhi na kuihakikishia damu mtiririko unaotakiwa kusambaa mwilini kwa uhakika zaidi.
Kitunguu maji ni chanzo kikubwa cha madini ya chromium yanayohitajika sana katika kazi ya kurekebisha kiwango cha sukari katika damu kwa kuziwezesha insulin kufanya kazi yake vizuri.
Dk. Mohamed Mkweli wa Kliniki ya Afya Bora anasema tafiti zilizowahi kufanywa zilibaini kuwa kitunguu maji kiwe kimepikwa au kibichi kinapofika kazini uwezo wake kiutendaji unabaki kuwa ni uleule japo kinapungua nguvu kidogo kikipikwa kwa vile baadhi ya ubora hupotea jikoni.
Anasema kuwa watafiti waliridhika na kukipa hadhi ya kuwa tiba kwa wagonjwa wa kisukari.
Anaendelea kueleza kuwa viini vyenye athari nzuri katika kitunguu maji ni Vitamin C inayozuia kukua kwa bakteria kwenye jeraha, ngozi.
Anasema kuwa pia ndani yake kunapatikana madini ya salfa, chuma na vitamini zinazotia nguvu mishipa.
Madhara
Kitunguu maji ni aina ya mboga ya yungiyungi, japo kina harufu kali inayochangamsha.
Anaeleza kuwa anayekitumia kitunguu maji anatakiwa ajihadhari kukitumia baada ya kukihifadhi kikiwa kimekatwakatwa, kwa sababu hufanya oksaidi na huwa kiini chenye sumu, kwa hivyo yatakiwa kitumiwe kikiwa freshi.
Tiba
Dk. Mkweli anasema imethibitishwa kisayansi kuwa juisi ya kitunguu maji huua vijidudu vya kinamasi na vya kifua kikuu, hufa baada tu ya kunusa moshi wake.
Anasema kuwa kitunguu maji kikitengenezwa kama kachumbari, ukali wake hupungua na hutia nguvu mwilini.
Pia anasema huongeza hamu ya kula na huimarisha misuli, hulainisha tumbo na kikipikwa na kuongezewa dawa nyingine husaidia na kuzidisha nguvu za kiume.
"Unajua kiungo hiki ni dawa sana kikitumika kwa kufuata ushauri wa daktari, kwani hufungua vizuizi mwilini, hutia nguvu za manii kwa mwanamke na mwanaume hasa kikipikwa kwa nyama, pia huondoa homa ya manjano," anasema.
Dk. Mkweli anasema ndani ya kitunguu maji kuna nguvu zaidi kuliko penisilini na hivyo hupoza kifua kikuu, kaswende na kisonono na huua aina ya vijidudu vya hatari.
Anasema kuwa magonjwa mengine yanayotibiwa na kitunguu maji ni pumu, uvimbe wa pafu, vidonda vya saratani, mvilio wa damu, majipu, chunusi, ukurutu, figo na vijiwe, kikohozi kwa wakubwa na wadogo, macho na pia hupunguza uzito.
Dk. Mkweli anawashauri watu wapendelee kutumia kitunguu maji kwa ajili ya kinga na tiba ya maradhi katika miili yao.
Na imethibitika kuwa wagonjwa wengi waliowahi kutumia tiba ya kitunguu maji kwa muda mrefu wamepata nafuu na wengine hupona kabisa maradhi yao.
Aidha, anasema na wale wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo ya nguvu za kiume wanashauriwa watafune kitunguu maji kibichi na kama tatizo litaendelea ni vyema kukutana na watibabu.
Kwa mgonjwa wa mapunye na kunyonyoka nywele kichwani Dk. Mkweli anasema wanaweza kujitibu kwa kukipondaponda vizuri, halafu wakachanganya na mafuta ya zaituni, kisha wakapaka kichwani hadi watakapoona tatizo limekwisha.
Lakini anamaliza kwa kusema wanaosumbuliwa na magonjwa makubwa kama figo, kisukari, shinikizo la damu ni vyema wakakutana na daktari ili kupata mchanganyiko wa dawa ambao ndani yake una kitunguu maji.