Snowden E
JF-Expert Member
- Apr 27, 2018
- 1,709
- 3,028
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli leo Jumapili Mei 3 amesema atatuma ndege Madagascar kwenda kufuata dawa ya mitishamba ambayo rais wa nchi hiyo anadai kuwa inatibu corona.
Magufuli amesema kuwa amewasiliana na Madagascar baada ya kupokea barua rasmi kutoka nchi hiyo iliyoeleza kuwa wamegundua dawa ya corona.
"Ninawasiliana na Madagascar na wameshaandika barua. Wanasema kuna dawa zimepatikana kule, tutatuma ndege kule na dawa zile zitaletwa pia ili Watanzania nao waweze kufaidika nayo… Sisi serikali tupo tunafanya kazi usiku na mchana."Rais Magufuli ameyasema hayo hii leo katika hafla fupi ya kumwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Augustine Mahiga aliyefariki Ijuumaa.
Hata hivyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya juu ya ubora wa dawa hiyo ambayo ni kinywaji kilichotengenezwa kwa mitishamba.
Matamshi yake yanajiri baada ya Rais wa Madagascar Andry Rajoelina kutangaza kwamba taifa lake limezindua dawa ya mitishamba ya kutibu Covid-19.
Ikizinduliwa kwa jina Covid-Organics, dawa hiyo ilitengenezwa kutoka kwa mmea artemisia (pakanga) - ambao ni mojawapo ya miti ambayo huchanganywa pamoja na mimea mingine ya Madagascar kama tiba ya ugonjwa wa Malaria.
Dawa hiyo ambayo imepakiwa kwenye chupa na kutangazwa kama chai ya miti shamba ilifanyiwa majaribio miongoni mwa watu wasiozidi 20 kwa kipindi cha wiki tatu, kulingana na katibu wa rais huyo Lova Hasinirina Ranoromaro aliyezungumza na BBC.