Dawa ya kiuno

Dawa ya kiuno

MAKOLA

Member
Joined
Jun 5, 2010
Posts
46
Reaction score
16
Wajumbe naumwa sana na kiuno mimi ni kijana wa kiume wa miaka 25 nitumie dawa gani
 
Pole mkuu. Maelezo yako ni mafupi kuweza kukupa ushauri mzuri zaidi ya kukushauri ukamwone daktari. Mara nyingi maumivu ya kiuno yanatokana na tatizo la prostatitis, ambayo inaweza kusababishwa na infection kwenye njia ya mkojo au sababu nyingine (non-bacterial). Hima kamwone daktari.
 
Pole sana ila huku kwetu ukisema unaumwa na kiuno mama atakukimbiza wewe! Hata hivyo wewe mwenyewe umeuliza kwa mitego eti una miaka 25! Kwa hiyo unafikiri dawa yake ni ile? kamwone daktari man!
 
Wakati unajipanga kwenda kumuona daktari, au kikombe cha babu, jaribu kutumia vifuatavyo:
1. Matango
2. Karoti
3. Pilipili hoho
Chukua vyote kwa pamoja tengeneza juice kama utaweza bila kuweka kiungo chochote wala kutoa maganda yake na dozi yake ni tunda moja kwa aina zote, pata asubuhi, mchana na jioni, ukivitafuna mojakwa moja na maganda ni bora zaidi. Hiyo ni tiba nzuri kwa maumivu ya kiuno na mgongo pia. Ukitumia siku ya kwanza una uhakika wa kupata nafuu kesho yake na ukiendelea wiki nzima tegemea kuto sikia tena maumivu kwa zaidi ya miezi 6. Zaidi ya hapo ikiwa ni utaratibu wako wa kula mara kwa mara basi tatizo hilo litafutika maishani. Tena kwa Tango hata nguvu za kiume humarika pia.
 
Kaka SaidAlly , hiyo tiba ni uhakika eeh? Yaani ulishaiexperience wewe mwenyewe?
 
Pia kuna tiba fulani hivi ya asili aliwahi kuielezea Mkuu Kisima. Sikumbuki vyema ila something like unamix tangawizi mbichi na mizizi ya ndulele unachua kiuno.
Ni kweli mixture hii ni suluhisho mujaarab kwa maumivu ya mgongo na kiuno.
Jaribuni kutumia wapendwa mpate kupumzika na hii kadhia.
 
Ni kweli mixture hii ni suluhisho mujaarab kwa maumivu ya mgongo na kiuno.
Jaribuni kutumia wapendwa mpate kupumzika na hii kadhia.

Hivi Mkuu, hii tiba ulishaiexperience wewe mwenyewe? Yaani uliitumia kabisa mwenyewe?
 
Hivi Mkuu, hii tiba ulishaiexperience wewe mwenyewe? Yaani uliitumia kabisa mwenyewe?
Ndiyo mkuu niliitumia yapata miaka mitano iliyopita. Maumivu niliyokuwa napata kipindi cha nyuma kabla ya hapo yalikuwa hayamithiriki. Tangu hapo yalifutika kabisa na ikitokea basi pengine ni kwajili ya uchovu utokanao na pilika za kutwa hiyo.

Mashuhuda wamo humu ambao pia iliwaletea matokeo chanya.
CC kassimneema
 
Back
Top Bottom