Dawa ya kuepuka kupigwa Ban hapa JF, hii hapa

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Ndugu zangu, wanajukwaa letu pendwa. Salaam!

Kila mara tunashuhudia humu mijadala mikali inayopelekea watu kurushiana maneno ya kejeli, dharau na wakati mwingine matusi. Mwisho wa yote, wanaojihusisha na lugha chafu wanajikuta wamepigwa ban – wengine kwa muda, wengine moja kwa moja, halafu wanaanza kulia eti Mods wanawaonea!?

Sasa leo nataka nieleze hapa dawa ya uhakika, ya kuzuia kupigwa ban humu.

Dawa ya kweli ya kuepuka kupigwa ban popote pale, hata mbinguni, ni hii: Kumcha Mungu na kutii sheria zake.

TULIA ndugu, usianze kunitafutia tusi. Endelea kusoma, utakubaliana na mimi mwishoni.

Kwa nini nimesema dawa ni Kumcha Mungu na kutii sheria zake?

Kwa sababu sheria za Mungu ni nyingi na pia ni kali. Nionavyo mimi, sheria za Mungu zinapita sheria za forums; zinapita sheria za barabarani, zinapita sheria za mitandao kama YouTube, Facebook nk. Kwahiyo ukimcha Mungu na kutii sheria zake zote, hutaona shida kutii sheria za JF, wala huwezi hata kuvunja sheria za nchi. Sheria za Mungu zinatufanya tuwe na maadili mema.

Angalia hapa baadhi ya sheria za Mungu:
"Usilipize kisasi, wala kuwa na kinyongo...bali umpende jirani yako kama nafsi yako."
(Mambo ya Walawi 19:18)

"Wasimtukane mtu yeyote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wawe wapole sana kwa watu wote."
(Tito 3:2)

Sasa fikiria: Ukitii sheria hizo za Mungu, JF Member akikukosea au kukutukana, huwezi kumrudishia tusi. Huwezi kukasirika kiasi cha kuvunja sheria za forum. Huwezi kuandika comments za kejeli.

Kama unashindwa kutii sheria chache tu za JF, ni ishara kuwa hata nje ya Forum hii, wewe ni mvunja sheria katika maeneo mengine ya maisha. Hali hiyo inaweza kukufanya upigwe ban ya milele – yaani, uzuiliwe kuingia kabisa mbinguni katika uzima wa milele!

Kuwa na "ignore list" sio suluhisho. Utam-ignore mtu kwa ku-tap/click "ignore" lakini moyoni utaendelea kumkumbuka. Pengine hata usiku utamuota ndotoni!

Ukimchukia mtu, hiyo chuki itaendelea kukutafuna na mwishowe kama nilivyosema, utapigwa ban ya milele usiingie mbinguni, kwenye uzima wa milele.

1 Yohana 4:20
"Mtu akisema kwamba anampenda Mungu, hali anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Maana mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hamwoni."
 
Binadam kama chiembe na lile zoba li tlaatlaah utaachaje kuyaporomoshea matusi? Ni heshima kubwa kuwatusi na kuwadhalilisha wachumia tumbo kama hao, kinyume chake kutofanya hivyo ni dhambi inayoweza kukupeleka motoni!
 
Kutokana na baadhi ya comment za hapo juu inaonesha Kuna watu hawawezi kupona kwa hii dawa

Tuendelee na majaribio
 
Ndugu zangu, wanajukwaa letu pendwa. Salaam!

Kila mara tunashuhudia humu mijadala mikali inayopelekea watu kurushiana maneno ya kejeli, dharau na wakati mwingine matusi. Mwisho wa yote, wanaojihusisha na lugha chafu wanajikuta wamepigwa ban – wengine kwa muda, wengine moja kwa moja, halafu wanaanza kulia eti Mods wanawaonea!?

Sasa leo nataka nieleze hapa dawa ya uhakika, ya kuzuia kupigwa ban humu.

Dawa ya kweli ya kuepuka kupigwa ban popote pale, hata mbinguni, ni hii: Kumcha Mungu na kutii sheria zake.

TULIA ndugu, usianze kunitafutia tusi. Endelea kusoma, utakubaliana na mimi mwishoni.

Kwa nini nimesema dawa ni Kumcha Mungu na kutii sheria zake?

Kwa sababu sheria za Mungu ni nyingi na pia ni kali. Nionavyo mimi, sheria za Mungu zinapita sheria za forums; zinapita sheria za barabarani, zinapita sheria za mitandao kama YouTube, Facebook nk. Kwahiyo ukimcha Mungu na kutii sheria zake zote, hutaona shida kutii sheria za JF, wala huwezi hata kuvunja sheria za nchi. Sheria za Mungu zinatufanya tuwe na maadili mema.

Angalia hapa baadhi ya sheria za Mungu:
"Usilipize kisasi, wala kuwa na kinyongo...bali umpende jirani yako kama nafsi yako."
(Mambo ya Walawi 19:18)

"Wasimtukane mtu yeyote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wawe wapole sana kwa watu wote."
(Tito 3:2)

Sasa fikiria: Ukitii sheria hizo za Mungu, JF Member akikukosea au kukutukana, huwezi kumrudishia tusi. Huwezi kukasirika kiasi cha kuvunja sheria za forum. Huwezi kuandika comments za kejeli.

Kama unashindwa kutii sheria chache tu za JF, ni ishara kuwa hata nje ya Forum hii, wewe ni mvunja sheria katika maeneo mengine ya maisha. Hali hiyo inaweza kukufanya upigwe ban ya milele – yaani, uzuiliwe kuingia kabisa mbinguni katika uzima wa milele!

Kuwa na "ignore list" sio suluhisho. Utam-ignore mtu kwa ku-tap/click "ignore" lakini moyoni utaendelea kumkumbuka. Pengine hata usiku utamuota ndotoni!

Ukimchukia mtu, hiyo chuki itaendelea kukutafuna na mwishowe kama nilivyosema, utapigwa ban ya milele usiingie mbinguni, kwenye uzima wa milele.

1 Yohana 4:20
"Mtu akisema kwamba anampenda Mungu, hali anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Maana mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hamwoni."
Umeongea utopolo
 
dawa ni kuivhukulia jf kama kiburudisho ukifungiw kush ukifunguliwa endeleza mapambano..... jf sio chakula
 
Ukishashiba mchunga wako unaandika lolote tuu linalokujia.....
 
Back
Top Bottom