Shida ni kuondoa myomas kwani naona ndiyo yanayobleed. Naelewa sana menopause na stage zoote nilishapitia.
i really doubt definition yako ya menopause(ambayo hujaisema ingawaje niliulizia hapo mwanzo)..Hata hivyo ningependa kusema,
Myoma
Ni aina ya uvimbe utokeao katika misuli, na ile itokeayo katika kizazi huitwa Uterine myoma...
Takwimu nyingi huonyesha kuwa tatizo hili la uvimbe hutokea kwa wanawake wenye umri wa kuweza kushika mimba(reproductive age),hata hivyo asilimia chache/ndogo sana hutokea kwa wale waliomaliza.
Dalili:
-Kukojoa(kwenda haja ndogo) mara kwa mara.
-Damu kutoka nyingi wakati wa hedhi au kati ya mzunguko na mzunguko.
-Maumivu makali sana wakati wa hedhi, maeneo ya tumbo na kiunoni (ingawaje maumivu wakati/kabla ya hedhi ni kawaida).
-Dalili za upungufu wa damu(kizunguzungu, kuchoka haraka, kuhisi mapigo ya moyo kwenda kasi isivyo kawaida).
-Mimba kutoka(kuharibika).
-Ugumba/utasa.
Vipimo mbali mbali vinaweza kufanyika na Picha ya tumbo (Abdominal Ultrasound) na USS za aina nyingine huweza kugundua aina ya uvimbe/vivimbe, ukubwa, sehemu gani vilipo katika tumbo la uzazi n.k
Tiba:
Njia za kupunguza/kuondoa vivimbe hutegemeana na aina ya uvimbe,tabia yake, umri wa mgonjwa, utashi wa kuweza kuwa na watoto, kama ana ugonjwa/tatizo jingine tofauti na hilo(mf.matatizo ya mfumo wa damu, moyo n.k)
Hivyo mgonjwa anaweza kupatiwa dawa(vidonge) bila upasuaji, dawa na kisha upasuaji au upasuaji moja kwa moja.
Ushauri:
Ni vyema kufanya uchunguzi hospitalini, na kupata elimu kutoka kwa daktari wako katika kuamua njia gani inayofaa KWAKO.