ONJO
JF-Expert Member
- Jun 1, 2022
- 216
- 265
Habari zenu wanajamii
Furaha yangu ni kupata majawabu ya kila swali.
Leo ninayo njia ya kuondoa udini serikalini.
Lipo neno linaitwa KWELI nalo ni mfano wa Biblia,na Quruan.Ila tofauti yake KWELI haitaji jina la mtume yeyote bali inafuata misingi,kanuni na sheria za nje.Hasa ikizingatia akili ya mtu mwenyewe,ili asiwe mtumwa katika jambo lolote.
Mfano wake angalieni thread niliyoandika.Tittle yake ni. ''Maisha na falsafa yake'' . Hapa utagundua kuwa KWELI hakuna wa kuipinga hata moja.Aliyepita,aliyepo wala atakae kuja.
Kama mungu atajalia proposal hii ifike serikalini.Basi serikali itakuwa na msahafu unaoitwa KWELI.Wakati huo wa kuapisha viongozi wetu watashika KWELI katika mkono wa kulia.
Kwa mfano Rais atatamka maneno haya.
''Mimi Samia S. Hasani Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Naapa kwamba nitaamini katika KWELI,nitaishi katika KWELI,na nitaitetea KWELI.Nitakuwa tayari wakati wowote kuirekebisha na kuiboresha katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kama KWELI itakavyoniongoza na kwa makubaliano ya watanzania wenzangu.Ee mwenyezi Mungu nisaidie''.
Hakuna njia zaidi ya hii ya kuiweka tanzania kuwa huru katika dini zake.
Na hapo tutakuwa na biblia,kweli na kuruani.Biblia zitabaki kwa wakristo,kweli itabaki serikalini na kuruani zitabaki kwa waislamu.
Kiongozi wa kweli atavutwa na KWELI kuliongoza taifa la tanzania maana kweli ina sifa ya kumwinua mtu wala hataletwa na dini bali na kweli isiyo na ubaguzi.
kwahiyo wanajamii ningependa kushauri. tuitafute hiyo kweli,ili iwe msahafu wa serikali
tujaze ufahamu na maarifa ndani yake.ili siku moja yeyote kati yetu akiwa kiongozi awasilishe wazo hili kwa viongozi wenzake.na wazo hili likipita ndilo litakaloondoa udini ndani ya serikali yetu.
Mimi nimewapeni utangulizi kupitia thread ya MAISHA NA FALSAFA YAKE kiasi kwamba tukiongezea vitu pale itafaa kutumika na hata ikisomwa na mtu yeyote asionekane wa kukosoa.Na hii itakuwa ya milele kwetu.
Nawasilisha.
Na ONJO mpenzi wenu.