Namna bora ya kudhibiti hasira
1. Tafuta chanzo cha hasira
Ni mambo gani yanakufanya kuwa na hasira? Ukishayajua tafuta namna ya kupata suluhisho la mambo hayo.
2.Epuka watu,maeneo, na mambo yanakufanya kupandwa na hasira
Pengine ni kwenye ushabiki wa mpira au labda ni kwenye majadiliano ya kisiasa, epuka mambo hayo.Si lazima ubishane kuhusu siasa au mpira,tafuta jambo lingine
3. Jifunze namna ya kudhibiti hisia zako
Hisia zinapaswa kuwa chini ya uwezo wako wa kuamua, si lazima kwa kuwa unahisi hasira basi ufanye mambo kwa hasira. Kwa kifupi tumia kichwa na sio fikara
4. Angalia/Tafuta namna bora za kutoa hisia za hasira
Wengi tumeshindwa hapa, si lazima ukiwa na hasira utoe matusi au maneno mabaya. Hamna haja ya kutaka kupigana au kutoa maneno ya kashfa,eleza kilichokuudhi bila kutumia hasira. '' When communicated respectfully and channeled effectively, anger can be a tremendous source of energy and inspiration for change.''
4. Jichunguze....
Jifanyie tathmini, je hasira zako zimetatua tatizo lolote? Je hasira inakufanya kuwa mtu bora mbele ya famlia yako, mke,mume na watoto.
Umeharibu urafiki mara ngapi kwa sababu ya hasira?
KIla la kheri mdau...