Dawa ya kutibu ugonjwa wa kuku kideri/kitoga/sotoka/mdondo/chinoya (Newcastle desease)

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,286
Reaction score
6,736
Wakuu namshukuru Mungu nimekuwa nikifanya utafiti wa magonjwa ya kuku
ambayo yanadaiwa kutotibika. Mimi sio daktari wa mifugo na wala sina taaluma
hiyo, utafiti wangu umekuwa wa kienyeji mno baada ya kukosa ushirikiano
kutoka kwa maafisa wa mifugo ambao mara kadhaa walitaka fedha au kunikatisha
tamaa.
Leo nakuja kifua mbele baada ya mchanganyo wa dawa ambao nimeufanya kuonekana
kuleta matunda kwa ugonjwa hatari wa kuku nilioutaja hapo juu. Katika utafiti wangu Jumla
ya kuku 22 wamekufa kutokana na majaribio mbalimbali ya dawa niliyokuwa nayafanya.
Lakini huu mchanganyo wa sasa umefanikiwa kuokoa maisha ya kuku 56 kati ya kuku 58
niliowajaribia.

Nawaombeni tuvute subira kwani mwezi wa 12. 2014 nitathibitisha kuwa ni dawa rasmi
au vinginevyo baada ya kukamilisha mambo machache ambayo yamesalia.
Mwisho Namshukuru MUNGU kwani haukuwa ujanja wangu isipokuwa ni Mwongozo wake.

AMANI KWENU.
 
kwahiyo ndo unaanza promo ya dawa yako au utatumwagia hapa huo mchanganyiko na sisi tunufaike?
 
Nitaweka tu mambo hadharani hakuna haja ya kuficha ficha kwani mchanganyo wenyewe
ni wa dawa za kawaida za binadamu.
 
Dah mkuu una maana dawa za hospitali au za kienyeji maana naona kama iko too chemically aiseeee....
 
Sio za kienyeji mkuu ni za hospitali.
 
Ase mi nilidhani dawa ndio tayari imeshapatikana kumbe ndio tusubiri mpaka dexemba
Mkuu humu JF wakati mwingine mnaleta hasira, unaweza kupost jambo la maana
ukakuta watu wanaanza kukudiscourage badala ya kuku encourage mfano angalia
baadhi ya michango kwenye thread yangu ya unataka kuwa tajiri? kule kwenye
ujasiriamali ambayo nimeeleza kwa kina juu ya ufugaji wa kuku wa kienyeji baadhi
ya michango ilinifanya nihamie kwenye MMU maana watu badala ya kushauriana wao
kazi yao ni kuponda tu.

Kimsingi hii dawa inayanya kazi vizuri kwa kuku wa kienyeji nimebakiza majaribio
kwa kuku wa kisasa nione utendaji wake, hapa huenda nikajikuta nikiua kuku
wengine kabla ya kufikia hitimisho la namna nzuri ya kutumia.
 
mimi ni mfugaji , nitakuwa wa kwanza kukusuport lakini dawa za madukani hazifai kabisa ni kimeo , sasa hivi natumia aloe vera
 
Mkuu humu JF wakati mwingine mnaleta hasira, unaweza kupost jambo la maana
ukakuta watu wanaanza kukudiscourage badala ya kuku encourage mfano angalia
baadhi ya michango kwenye thread yangu ya unataka kuwa tajiri? kule kwenye
ujasiriamali ambayo nimeeleza kwa kina juu ya ufugaji wa kuku wa kienyeji baadhi
ya michango ilinifanya nihamie kwenye MMU maana watu badala ya kushauriana wao
kazi yao ni kuponda tu.

Kimsingi hii dawa inayanya kazi vizuri kwa kuku wa kienyeji nimebakiza majaribio
kwa kuku wa kisasa nione utendaji wake, hapa huenda nikajikuta nikiua kuku
wengine kabla ya kufikia hitimisho la namna nzuri ya kutumia.

Mkuu nilipoona heading nilijua dawa tayri imepatikana na ndicho nilichosema, sikuwa nina lengo la kukatisha tamaa, ikipatikana dawa hii nami itanisaidia kwani nami pia nafuga-nisamehe kama nime sound vibaya, halikuwa lengo langu!!
 
Ooh. Samahani mkuu pengine umejisikia vibaya kwa kutonielewa
kauli yako nimeielewa vema na wala haina tatizo nilichokusudia ni
kuwa nashindwa kuinadi mapema kutokana na aina ya watu niliowatja
kwani wengine wataanza kuponda na kusema Mfano. Kwanini
umekurupuka badala ya kumaliza utafiti kwanza na kwa kuku wa kisasa.
Nilikuelewa ndio maana nilikupa mfano wa watu wenye tabia hizo
na sio wewe.
 
Mods, mmeileta huku kana kwamba mimi nataka kufanya biashara ya hiyo
Dawa? Nikishakamilisha hayo majaribio nitaitangaza bila gharama yoyote
labda mtu mwenyewe ambaye itamsaidia si vibaya kama ataamua kutoa
shukrani.

Narudia sikusudii kuuza hiyo dawa.
 
mkuu umefikia wapi katika utafiti wako?
 
Nadhani hata super gro inasaidia katika kutibu ugonjwa wa Newcastle kwa kiwango cha juu sana wadau
 
Mods, mmeileta huku kana kwamba mimi nataka kufanya biashara ya hiyo
Dawa? Nikishakamilisha hayo majaribio nitaitangaza bila gharama yoyote
labda mtu mwenyewe ambaye itamsaidia si vibaya kama ataamua kutoa
shukrani.

Narudia sikusudii kuuza hiyo dawa.

Nasubiria kwa hamu.....bado miezi kadhaa tu kufika desemba, 2014.
 
Wakuu namshukuru Mungu nimekuwa nikifanya utafiti wa magonjwa ya kuku
ambayo yanadaiwa kutotibika. Mimi sio daktari wa mifugo na wala sina taaluma
hiyo, utafiti wangu umekuwa wa kienyeji mno baada ya kukosa ushirikiano
kutoka kwa maafisa wa mifugo ambao mara kadhaa walitaka fedha au kunikatisha
tamaa.
Leo nakuja kifua mbele baada ya mchanganyo wa dawa ambao nimeufanya kuonekana
kuleta matunda kwa ugonjwa hatari wa kuku nilioutaja hapo juu. Katika utafiti wangu Jumla
ya kuku 22 wamekufa kutokana na majaribio mbalimbali ya dawa niliyokuwa nayafanya.
Lakini huu mchanganyo wa sasa umefanikiwa kuokoa maisha ya kuku 56 kati ya kuku 58
niliowajaribia.

Nawaombeni tuvute subira kwani mwezi wa 12. 2014 nitathibitisha kuwa ni dawa rasmi
au vinginevyo baada ya kukamilisha mambo machache ambayo yamesalia.
Mwisho Namshukuru MUNGU kwani haukuwa ujanja wangu isipokuwa ni Mwongozo wake.

AMANI KWENU.

kaka ukifanikiwa nitakuwa wa kwanza kukunga mkono mkuu! hongera sana
 
Back
Top Bottom