Dawa ya kutoa chale

Chemwali

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2011
Posts
397
Reaction score
178
Eti kuna dawa ya kutoa chale zile za mgongo au sehemu nyingine ya mwili?
 
Niletee mkojo wa mtu aliyekuchanja hizo chale, magadi robo kilo, yai moja la mjusi wa mwambani, ubani wa Pemba na maji ya mto Yordani. Ukivipata hivyo, chale kwisha

Pole sana mkuu.
 
Mkuu nenda pale S.H Amon kwenye picha ya askari, I hope makovu ya mwili yana solution
 
Niletee mkojo wa mtu aliyekuchanja hizo chale, magadi robo kilo, yai moja la mjusi wa mwambani, ubani wa Pemba na maji ya mto Yordani. Ukivipata hivyo, chale kwisha

Pole sana mkuu.
Kweli Mwana mtoka pabaya umedhihirisha ulikotoka,je akivipata afanye nini ili ziishe? Maana suala pekee si kuvipata hivyo ulivyomwambia bali kuondoa chale
 
sm serious jamani nazichukia du
 
sm serious jamani nazichukia du

Pale nimekutania tu binamu. Nenda S.H Amon, nakumbuka siku moja nilienda pale kununua dawa, dada mmoja kati ya wale masupeshalist akaniona na kovu mkono wangu wa kushoto akaniambia siku nikiliona kero nisisite kumuona aliondoe.

Nenda pale naamini utafanikiwa kwa kuwa mimi kovu langu ni kubwa mara 150 zaidi ya ukubwa wa chale. Kama aliona kovu linaweza kuwa wipid aut, sembuse chale.

Lkn 'demu mwenyewe ulimpata mkuu?'
 
Eti kuna dawa ya kutoa chale zile za mgongo au sehemu nyingine ya mwili?

hee unazo mkuu ..... wanawake wengi sana kwenye daladala wanakuwa na hizo chale, nahisi ni kazi za yule mbunge wa ccm mh. ngojani maarufu kwa jina la prof. maji marefu!!!!
 
Kweli Mwana mtoka pabaya umedhihirisha ulikotoka,je akivipata afanye nini ili ziishe? Maana suala pekee si kuvipata hivyo ulivyomwambia bali kuondoa chale

Ah, na wewe St. Joseph mbona hunielewi? Aje navyo kwangu mimi ndio fundi mwenyewe. Ila nasikitika kwamba itabidi nimchanje chale ili kuondoa chale.

Nimetoka Nigeria kuongeza ujuzi si muda mrefu
 
Last edited by a moderator:

taratibu mkuu ...... mbona unauliza sasa kwa sauti???
 
hee unazo mkuu ..... wanawake wengi sana kwenye daladala wanakuwa na hizo chale, nahisi ni kazi za yule mbunge wa ccm mh. ngojani maarufu kwa jina la prof. maji marefu!!!!

sio wanawake tu siku hizi watu kibao,,mabrothermen kwa masista duu nadhani wazazi walituponza..then nw wameokoka sasa kivumbi alama tuloachiwa..kuna mhubiri alisema kwenye chale hiyo maaana yake NI AGANO NA SHETANI LA NITAKUPENDA HADI KUFA DU
 
Ah, na wewe St. Joseph mbona hunielewi? Aje navyo kwangu mimi ndio fundi mwenyewe. Ila nasikitika kwamba itabidi nimchanje chale ili kuondoa chale.

Nimetoka Nigeria kuongeza ujuzi si muda mrefu
Chemwali umemsikia mganga mpya toka Nigeria?Anatoa chale kwa kuchanja chale kwa maana ya bandika bandua
 
hee unazo mkuu ..... wanawake wengi sana kwenye daladala wanakuwa na hizo chale, nahisi ni kazi za yule mbunge wa ccm mh. ngojani maarufu kwa jina la prof. maji marefu!!!!

Lakini sisi kina Nchumali, Chimwale, Chikapu, Chigala na Honi tunachanjwa kwa mila zetu. Gesi ikianza kuchimbwa tutajiocha chura jetu na gesi bha!

Ukimuona big show usoni ndio utanielewa
 
Last edited by a moderator:
Chemwali umemsikia mganga mpya toka Nigeria?Anatoa chale kwa kuchanja chale kwa maana ya bandika bandua

Yeye hataki za mgongoni, mimi nitamchanja kwa mtindo ule Deadstone Lusinde alisema CDM wamechanjwa na Maji Marefu (Kwenye Didas Mas.b..i)
 
Atoe tangazo hata humu JF aone atakavyopata soko..nguo zinaficha mengi..heri mimi nina 2 tu wengine..kama chain...tena zinaonekana hata ajifanye mzungu lakini zinaning'inia shingoni inashusha P kweli
 
sio wanawake tu siku hizi watu kibao,,mabrothermen kwa masista duu nadhani wazazi walituponza..then nw wameokoka sasa kivumbi alama tuloachiwa..kuna mhubiri alisema kwenye chale hiyo maaana yake NI AGANO NA SHETANI LA NITAKUPENDA HADI KUFA DU

kweli kiimani hizo chale ni maagano mkuu!!!!
'ila maagano yanaondolewa kiroho mkuu!!
 
sio wanawake tu siku hizi watu kibao,,mabrothermen kwa masista duu nadhani wazazi walituponza..then nw wameokoka sasa kivumbi alama tuloachiwa..kuna mhubiri alisema kwenye chale hiyo maaana yake NI AGANO NA SHETANI LA NITAKUPENDA HADI KUFA DU

Dada yangu vya kuambiwa changanya na zako... hivi lile kovu la sindano ya chanjo begani, nalo ni agano la shetani?
Wataalamu wa kienyeji hawakuwa na singano za kuchoma dawa, hivyo kama dawa si ya kunywa na ilitakiwa iingie mwilini moja kwa moja, walikuwa wanakata kidogo na kuipaka. Hakuna uhusiano wowote kati ya shetani na chale... na hizi dawa za mimea tunazoziita za shetani leo, ndizo zilizowapa afya wazee wetu hadi wakatuzaa, kabla hazijaja sindano na vidonge vya wazungu.

Tusipuuze utamaduni wetu, tukatukuza wa wageni...
 
Yeye hataki za mgongoni, mimi nitamchanja kwa mtindo ule Deadstone Lusinde alisema CDM wamechanjwa na Maji Marefu (Kwenye Didas Mas.b..i)
Ha ha ha ha Mwana mtoka pabaya nimekukubali ila sidhani kama CDM wanaweza kukubali chale za Maji Marefu labda wawe wamekufa
 
Atoe tangazo hata humu JF aone atakavyopata soko..nguo zinaficha mengi..heri mimi nina 2 tu wengine..kama chain...tena zinaonekana hata ajifanye mzungu lakini zinaning'inia shingoni inashusha P kweli
Sisi ni waafrika na chale ni tamaduni zetu,ukiangalia sana ni watanzania wachache sana ambao hawana chale na hawa ni wale wa kizazi cha dot com ila sisi wa zamani chale izilikuwa hazikwepeki na mbaya zaidi wengine zilikuwa zinachanjwa sehemu ambazo huwezi kuficha.Nakumbuka siku moja ilibidi nipigwe chale ya ulimi du!Hapo uzalendo wa imani za kimila ulinishinda nikasema kama hakuna dawa nyingine zaidi ya kunilima hiyo chale basi sitaki.
Kuna mdau humu kashauri uende S H Amon pale maeneo ya Samora,inaweza kusaidia namna ya kuondoa matatizo uliyonayo,jaribu kote kote ila kwa Mwana mtoka pabaya ingekuwa mimi ningeogopa.
 
Thanks kwa ushauri..but kwa kuanza tu hiyo picha yako hapo pembeni ungeweka ya Mwaikimba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…