Mkuu chama 2 chawa,
Kabla ya kuamua kufanya hayo yote ni lazima moyo wako ukubali kufanya hayo maamuzi uliyoamua,
Ngoja nikupe mfano kuhusu mimi,
Katika maisha yangu nimejikuta nimefanya kila kitu kulingana na mazingira yangu hivyo sijaona kigeni bado, hata wanawake nimetembea nao mpaka nikachoka nikafanya kila aina ya starehe na uchafu lakini mwaka huu mwezi wa 8 nikasema sitaki kujihusisha na mapenzi ya aina yoyote hao wanawake kwa sasa nikikaa nao napiga nao stori na kushirikiana mambo ya kijamii, kiuchumi n.k
Sina hata chembe za hisia juu yao hata kama wakiwa hawana nguo mwilini mwao bado nawaona wa kawaida ni kweli ukiwatizama ni wazuri wamejaliwa si rahisi kwa mwanaume rijali kukaa nao bila kuwatongoza wala kuwatamani kwa jinsi walivyo umbika,
Unajua ni kwanini ni kwasababu nilisha " set " akili yangu kuwa sihitaji hisia yoyote na mwanamke hata awe mzuri vipi lakini si kwa milele ila kwa muda mfupi tu yaweza kuwa miaka 5 au 10, hii itakusaidia katika kipindi hicho kufanya mambo yako ya muhimu na ukiwa " serious " utajikuta umepiga hatua ndefu sana katika maisha yako "either" kiuchumi, kielimu, na kadhalika...
Huo muda wa kuzuia hisia ndiyo muda mzuri wa kufanya mambo ya maana na kwa akili zaidi,
Punguza kufanya matumizi makubwa, unywaji wa pombe , uvutaji wa sigara, na mambo yasiyo na msingi kiafya na kimaendeleo baada ya miaka 5 au 10 unaangalia je nimefanya hayo yote kwa kujinyima na sasa ni hatua gani niliyofikia ya mafanikio ukiona upo vizuri basi ni wazi ya kwamba unarudisha hisia zako na kufanya mambo yako kama kawaida ila kwa uangalifu na unakini mkubwa kusudi usije kupotea tena.
Hivi ndivyo nilivyo panga kufanya, kamwe huwezi kutoa hisia milele ila kwa kitambo tu.........