Dawa ya kuzuia tumbo sugu la kuunguruma na kunyonga

Dawa ya kuzuia tumbo sugu la kuunguruma na kunyonga

Chele2

Senior Member
Joined
Apr 5, 2013
Posts
102
Reaction score
5
Jaman jf doctors nina tumbo la kuunguruma kwa muda mrefu sasa,kama miaka 8,mpaka mwaka jana nlipoanza kutumia dawa,lakin hakuna mafanikio,naomba anayejua dawa anisaidie ninunue
 
Tumia aloe vera gel ni hautakaa usikie tena hilo tatizo.
 
Tumia aloe vera gel ni hautakaa usikie tena hilo tatizo.

Mimi hii ilisaidia sana kutuliza lakini baada ya kumaliza kile kidumu kimoja mambo yakarudi palepale.
Cha kushangaza nikiwa nje ya nchi na nikae kwa mda tatizo linakua na dalili ya kuisha lenyewe!
 
Sasa mbona nabak njia panda? ina maana hata aloe vera gel pia siyo ya uhakika?
 
Sasa mbona nabak njia panda? ina maana hata aloe vera gel pia siyo ya uhakika?

Tumia kitunguu swaumu. Menya punje kama sita zikate zikate then meza na maji kama vidonge Meza mara moja kwa siku tatu. Itaisha kabisa. Poleee!!
 
Chele2, Nyamgluu mimi nilikuwa tatizo hilo kwa takribani miaka 10,nikasoma thread za MziziMkavu za kutumia maji ya moto na asali,nilichokifanya mimi ni kuwa nakunywa maji ya uvuguvugu(moto)asubuhi kabla sijala chochote glasi 2,baada ya chai kama nusu saa nakunywa glasi 1 na kila baada ya kula chakula huwa nakunywa maji ya moto na ya mwisho nainywa baada ya chakula cha usiku,nimefanya hivyo kwa miezi 2 mfulululizo na tatizo limekwisha kabisa yaani hivi ninavyokwambia nina raha ya ajabu maana mimi tumbo lilikuwa mpaka linajaa gesi na kunisababishia kujamba mara kwa mara kitu ambacho ilikuwa ni kero kubwa sana kwangu.Nakushauri ujaribu hii kwani mimi nilikwenda mpaka kwa kina Rahabu nikijua nina vidonda vya tumbo nilichoambulia ni kuliwa hela na sikupona.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom