PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,199
- 8,761
Wadau wa Jukwaa la JFD,
Napenda kuwajuza kuwa sasa hivi kuna hatari kubwa ya watu kupata mgogoro mkubwa zaidi wa kiafya kuhusiana na uingizwaji wa madawa ya kila aina nchini kwetu.
Sasa hivi kuna dawa toka Kenya iliyosambaa kwenye maduka ya Dawa(hasa huku Arusha) inayodaiwa kuongeza nguvu za Kiume, inauzwa kama njugu, na wenye maduka ya dawa kwa sasa hivi inawatajirisha. Sikujua kama shida ya nguvu za kiume kwa watu imekuwa ya juu kiasi hiki katika miaka hii, hadi watu kuamua kunywa dawa ambayo hata packaging yake inatia mashaka kiasi hicho!
Naomba kufahamu kwa wataalamu, je dawa za aina hii zimehakikiwa na Idara zetu za viwango vya madawa, na kuthibitishwa na mamlaka ya vyakula na Dawa?
Tusije tukawa tunatibu shida ya leo, huku tunaangamiza kizazi cha miaka 20 ijayo!
Nawahofia sana wanangu!
(Pichani: mfuko wa dawa hiyo inayoitwa Alvoy toka Kenya).