Dawa ya Libido toka Kenya.

Dawa ya Libido toka Kenya.

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,199
Reaction score
8,761
Wadau wa Jukwaa la JFD,

Napenda kuwajuza kuwa sasa hivi kuna hatari kubwa ya watu kupata mgogoro mkubwa zaidi wa kiafya kuhusiana na uingizwaji wa madawa ya kila aina nchini kwetu.

Sasa hivi kuna dawa toka Kenya iliyosambaa kwenye maduka ya Dawa(hasa huku Arusha) inayodaiwa kuongeza nguvu za Kiume, inauzwa kama njugu, na wenye maduka ya dawa kwa sasa hivi inawatajirisha. Sikujua kama shida ya nguvu za kiume kwa watu imekuwa ya juu kiasi hiki katika miaka hii, hadi watu kuamua kunywa dawa ambayo hata packaging yake inatia mashaka kiasi hicho!

Naomba kufahamu kwa wataalamu, je dawa za aina hii zimehakikiwa na Idara zetu za viwango vya madawa, na kuthibitishwa na mamlaka ya vyakula na Dawa?

Tusije tukawa tunatibu shida ya leo, huku tunaangamiza kizazi cha miaka 20 ijayo!
Nawahofia sana wanangu!

(Pichani: mfuko wa dawa hiyo inayoitwa Alvoy toka Kenya).
DSC01047.JPGDSC01048.JPGDSC01051.JPG
 
Hizi ni dawa za kukwepwa kama ukoma hadi hizo mamlaka husika zithibitishe. Tabu watu wengi tunafikiri kila kilicho dukani/katika pharmacy ni halali.
 
Mkuu Pakajimmy huko kwenu Arusha kuna Serikali inayofuatilia hayo madawa yanayotoka Kenya au kuna Serikali hewa ?

attachment.php
 
Msipoacha ujuha na ulimbukeni mtaumizwa sana na wasasi wa ngawira. Hakuna kitu kama hicho hata hiyo Viagra na matatizo matupu. Ni suala la kutumia akili.
Wadau wa Jukwaa la JFD,

Napenda kuwajuza kuwa sasa hivi kuna hatari kubwa ya watu kupata mgogoro mkubwa zaidi wa kiafya kuhusiana na uingizwaji wa madawa ya kila aina nchini kwetu.

Sasa hivi kuna dawa toka Kenya iliyosambaa kwenye maduka ya Dawa(hasa huku Arusha) inayodaiwa kuongeza nguvu za Kiume, inauzwa kama njugu, na wenye maduka ya dawa kwa sasa hivi inawatajirisha. Sikujua shida ya nguvu kwa watu sas

Naomba kufahamu kwa wataalamu, je dawa za aina hii zimehakikiwa na Idara zetu za viwango vya madawa, na kuthibitishwa na mamlaka ya vyakula na Dawa?

Tusije tukawa tunatibu shida ya leo, huku tunaangamiza kizazi cha miaka 20 ijayo!
Nawahofia sana wanangu!

(Pichani: mfuko wa dawa hiyo inayoitwa Alvoy toka Kenya).
View attachment 75012View attachment 75013View attachment 75014
 
Malawi kuna waziri mzima tena wa afya alizimia Hotelini hivi karibuni akiwa na kibinti cha Sekondari - kisa alijioverdoze viagra - jamii ya hizo Libido.
 
Malawi kuna waziri mzima tena wa afya alizimia Hotelini hivi karibuni akiwa na kibinti cha Sekondari - kisa alijioverdoze viagra - jamii ya hizo Libido.
Broda pmwasyoke
Je iliwekwa wazi au walisema ni Shinikizo la Damu?
 
Last edited by a moderator:
Broda pmwasyoke
Je iliwekwa wazi au walisema ni Shinikizo la Damu?

Tangu Rais wa mwisho afariki magazeti yana uhuru ulioongezeka wa kuanika matukio kama haya na kuyaripoti kiukweli. Kigogo alishindwa kuinfluence waripoti uwongo kuhusu sababu ya kuzimia na kuhusu binti wa sekondari.
 
Issue ilikuwa magazetini wazi kabisa - Mheshimiwa kawa disgraced vibaya.

Tangu Rais wa mwisho afariki magazeti yana uhuru ulioongezeka wa kuanika matukio kama haya na kuyaripoti kiukweli. Kigogo alishindwa kuinfluence waripoti uwongo kuhusu sababu ya kuzimia na kuhusu binti wa sekondari.
Huyo Waziri bado yupo ofisini hadi leo?
 
"Mtu yeyote ambaye hatafanya kitu chochote, ataishi, na hatimaye atakufa bila kufanya kitu chochote" Mtu ana tatizo, mambo hayaendi sawa, dawa ameiona, je! utamzuia asitumie dawa, wakati ana tatizo???????? cha msingi, tafuta njia mbadala kwa tatizo hili, kwani tatizo la libido ni kubwa sana sasa hivi kwa rika zote, na serikali yetu sikivu, haioni kama kuna tatizo, kwani ukienda hospitali za umma jibu lake ni rahisi tu, kwani unaambiwa punguza mawazo, wakati nyumbani huna sukari, sijui kama unaweza kupunguza mawazo wakati mambo nyumbani ni vurugu tupu. "ACHA TUTUMIE MADAWA, KWANI MWISHO WA MAISHA NI KIFO TU" na hii ni kwa kila mja, utumie au usitumie.
 
Ndiyo tabu ya nchi zetu mtu hata akiwa na miskendo hawajibiki kwa kujiuzulu wala nini. Bado yupo na aliishia kusema story nzima ni set up ya wasiompenda.
Ha ha haaaa!
"LIKE A NEIGHBOR, LIKE A NEIGHBOR"
 
Back
Top Bottom