Dawa ya mafua ya kuku

Dawa ya mafua ya kuku

Wakuu habari za muda huu,naomba kama Kuna mtu anajua dawa ya kuwapa kuku wenye mafua.
Wanakohoa na kusinzia.
Natamani kujua dawa yoyote,hata kama ni za miti.
Ni kuku wa kienyej
Natanguliza shukrani
Nafahamu kuna bird flu (coryza), pia kusinzia bird cold tumia antibiotics kama tetracycline, amoxicillin kwenye maji kagua mazingira wanayolala kuku wako yasiwe na unyevu(high humidity) watapona baada ya mwezi hivi au zaidi kama ni vifaranga wanaweza hata kufa kama hawatokula vizuri.

Kwa magonjwa mengi ya kuku huwa wanapona lakini bado wanakuwa carriers(yaani wanabeba ugonjwa) kwa hiyo kama una kuku wengi ni vyema zaidi kuwatenga waliohudhurika kwa kuwaua maana huwa wanadumaa baada ya kupata ugonjwa na kama ni layers hawatokupa idadi nzuri ya mayai.
 
Nafahamu kuna bird flu (coryza), pia kusinzia bird cold tumia antibiotics kama tetracycline,amoxicillin kwenye maji kagua mazingira wanayolala kuku wako yasiwe na unyevu(high humidity) watapona baada ya mwez hiv au zaid kama ni vifaranga wanaweza hata kufa kama hawatokula vizur. Kwa magonjwa mengi ya kuku huwa wanapona lakini bado wanakuwa carriers( yaan wanabeba ugonjwa) kwa hiyo kama una kuku wengi ni vyema zaidi kuwatenga waliohudhurika kwa kuwaua maana huwa wanadumaa baada ya kupata ugonjwa na kama ni layers hawatokupa idadi nzur ya mayai
Asante Sana boss
 
Wakuu Asanteni kwa ushauri,nkmefanikiwa kupata dawa km alivyonielekeza mkuu hapo juu.
Condition nyama yake isiliwe Hadi siku 15 ziishe,mayai nayo yasitumike na binadamu.
Ni dozi ya siku tano,nitawapa mrejesho Mungu akijalia.
Nawatakia kila la kheri ktk kuusakanya mkate
 
Ngoja nipambane nihakikishe wanapona,hapa ni Hadi kieleweke.
Ila miaka ya nyuma kuku wa kienyej I hawakuwa wakishambuliwa na magonjwa km Sasa.
Mhhhh
Kama ni kienyeji ana ishi ndani ya banda bila kutoka lazima awe na changamoto kama wa kisasa ila kama anaishi kama ilivyo zoeleka basi huwa hawana changamoto hizo
 
Kama ni kienyeji ana ishi ndani ya banda bila kutoka lazima awe na changamoto kama wa kisasa ila kama anaishi kama ilivyo zoeleka basi huwa hawana changamoto hizo
Wako ndani muda mwingi wakati huu wa msimu ,watu wameshaanza kuotesha mashambani hivyo ukiachia kuku ni ukorofi kwa wengine
 
Wakuu Asanteni kwa ushauri,nkmefanikiwa kupata dawa km alivyonielekeza mkuu hapo juu.
Condition nyama yake isiliwe Hadi siku 15 ziishe,mayai nayo yasitumike na binadamu.
Ni dozi ya siku tano,nitawapa mrejesho Mungu akijalia.
Nawatakia kila la kheri ktk kuusakanya mkate
kwakua n kienyeji jitahidi uwe unawapa dawa za kienyeji mara kwa mara (kwa kuwachanganyia kwenye maji au chakula) kwani huwa inasaidia sana kwa magonjwa nyemelezi na inasaidia kuepusha vifo vya mapema wapatavyo magonjwa
 
Asante kwa ushauri boss,nitazingatia
 
Back
Top Bottom