Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,308
Je, pia inawezekana aliambiwe atoe bure na kwa sababu ya hali ngumu ya maisha akaanza kutoza pesa na kudai Mungu alimwamuru na bei ya dawa zake?
tusijidangaye wapendwa, Mungu wa kweli haponyi namna hiyo ya samunge
hakuna aliyepona, sasa utapata wapi vyeti vinavyothibitisha uponyaji?
kweli jeshi lote lililoenda samunge hadi leo wakiwemo wanaJf wote hawa, tumekosa hata ushuhuda mmoja tu wa kuaminika? mbali na hadithi tu za fulani kapona?
Muanzishaji mada anataka kujihakikishia kama watu wanapona kweli huko kwa babu. Wote wanaotoa majibu hapa na kubishana hakuna anayejibu shali. Mimi napenda kumpa changamoto aliyeanzisha mada kwamba hapa huwezi kupata jibu lolote lile ambalo unaweza kuridhika nalo. Kila familia ina wagonjwa hivyo inakubidi wewe mwenyewe ufanye research - peleka mgonjwa ambaye unamfahamu akapate kikombe, akirudi utakuwa unamfuatilia kujua kama amepona kweli au la. Wengi wanaokwenda kupata kikombe huwa hawatoi ushahidi kama wamepona au bado hawajapona kwa sababu wengi wanaenda kule kwa siri na wasingependa maradhi yao kufahamika. Sasa akisema mimi ni fulani nilikuwa naumwa kitu fulani atakuwa amejitangaza tayari.
Kuna watu mimi ndugu zangu wamepona, sitaweza kuwataja hapa kwani hawatapenda. Pia mtu akikupa ushuhuda kwamba aliumwa na baada ya kikombe cha babu amepona utaweza kuthibitisha hayo? Si rahisi kwa sababu humjui mtu huyo kama aliumwa kweli au anaongopa.
Ushauri mwingine wa kukuwezesha kuamini ni kwamba kuna kikundi ambacho kimejitangaza kinaishi na virusi vya ukimwi, tayari kimepelekwa kwa babu na kupata kikombe. Kilijitangaza kwenye TV kwa sababu viko vikundi hivi vinafahamika. Wameahidi watakuwa wanatoa taarifa ya maendeleo yao baada ya kipindi fulani sikumbuki - hii ndiyo inaweza kuthibitisha kama watu wanapona au hawaponi. Kwa vile huumwi vuta subira utajihakikishia si muda mrefu.
Watu wengi walienda kwa Babu kwa imani kwamba ametumwa na Mungu wa mbinguni muumba wa mbingu na inchi, labda ungetusaidia kweli alitumwa na Mungu? otherwise, ata shetani(mungu wa dunia hi) naye anaponya!
Mimi nashaangaa sana, Kozi nimepita leo hapo Bunda nikiwa nakuja hapa Singita grumeti nimeona msururu wa mabasi makubwa na madogo ukiwa unasubili kwenda loliondo,
sasa kama kweli hawaponi nini kinawasukuma hawa watu kwenda huko.
sheikh yahaya tu ndiye anayeweza kuzuia kifo.........au sio????
Nini Yahaya, hata akitokea Muislamu mwingine ambaye atakuwa na madai kama ya huyo babu wa kanisa, basi madai yake hayatokubaliwa na yatakuwa batili hata kama atayaegemeza na Uislamu. Hakuna wa kuoteshwa wala kuletewa ufunuo hivi sasa. Hizo ni njia za kitapeli za kujitafutia umaarufu na utajiri wa njia ya mkato. Na wajinga ndio waliwao.
Watu waongo, wajanja, malaghai wa namna hiyo wanaodai kuoteshwa, wenye malengo ya kutafuta umaarufu, utajiri au kutangaza dini zao kwa njia kama hizo za kudai kuoteshwa, hawajaanza leo, na wataendelea kutokeza wengi.... Na watawapoteza wengi.
Sijaona tatizo kwenye dawa ya babu! iko ok na sio sahihi kuifananisha na Kinjekitile, rejea ripoti ya Muhimbili! tutaongea baadae
Kweli mkuu. Jana magazeti yamesema kuna magari manne kutoka Kenya yametua Loloindo. Kama waKenya waliokunywa kikombe wangekuwa hawajapona wangekuja?
Ndg: rejea maoni yangu, ujue nini uponyaji wa Mungu aliye hai. Tatizo ni ndoto yake na masharti yake. Si kuponya.! Kwani hata Lazaro aliye fufuliwa na Yesu bado yu hai? Hao waliotibiwa na babu wamepona kwa imani gani? Kama ni ya Mungu aliye hai si sawa. Kama ni utafit wake sawa. Soma neno. Usitumie akili tu.Mimi nipo loliondo si magari manne tu kutoka kenya kuna magari zaidi ya mia yanapita kila baada ya siku tatu hayo magazeti hayana ukweli
Watu wanashindwa kuelewa kuwa siku dawa ya UKIMWI ikipatikana dunia yote itageuka upside down. Itakuwa ni habari moja kubwa sana kati ya habari zilizowahi kuvunja rekodi humu duniani. Si Tanzania tu peke yake bali the whole world will be in shock.