Dawa ya mchwa ni ipi?

Kichwa Ze Don

Senior Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
198
Reaction score
321
Rejea kichwa habari hapo juu,

Napenda kujua ni dawa ipi nzuri ambayo naweza kutumia maana na site yangu kuna chumba kimoja kinasumbuliwa na mchwa nichatumia ma oil mixture petrol nikachanganya na nikapiga rough floo lakini naona wameanza upya, je ni dawa ipi nzuri naweza kuitumia kumaliza tatizo hili?
 
TwigaPrid yenye imidacloprid, utanishukuru
 
Mkuu,Nenda Duka la pembejeo za kilimo na mifugo,omba Sumu inayoitwa Duduba450EC, Changanya 40mls kwa 20 lts of water,Piga Mara tatu,Hakika utamaliza shida,binafsi huwa naziuza
 
Mkuu Ulifanikiwa kupata Dawa ya uwakika? Na me nina changamoto iyo
 
Ipo moja imekaa kibishi ila ni yenyewe unakuwa unatumia shombo la dagaaa kumwaga eneo husika kwa mara kadhaa wanaisha wote
 
Kuna moja inaitwa TERMITE KILLER hiyo nayo inasaidia sana. Nunua lita moja TZS 35K - 40K. Chimba nje kwa kufuatisha msingi kama sm 50 hivi kwenda chini, changanya cc 30 kwa lita ishirini, mwanga kwenye hilo shimo ulilo chimba kama lita ishirini za mchanganyiko kwa mita 5-7 hivi hapo chini, unakuwa umemaliza kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…