Dawa ya meno ya kufanya yawe meupe na kung'arisha

Dawa ya meno ya kufanya yawe meupe na kung'arisha

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Wadau mimi ni mshkaji fulani wa kibongo mweusi. Sio black. Ni mweusi, kama hujui tofauti mwangalie aliyekuwa Rais wa USA Barack Obama ile rangi yake. Walimwita Black.

So naposema mimi mweusi uelewa mweusi huku kwetu anakuaje. Nina mahitaji makubwa mawili naomba mnisaidie.

1. Napenda sana meno meupe kama unga uliokobolewa, meupe peeee. Je nitumie dawa gani ya meno ili kung'arisha.

Ukiacha habari za kwenda Hosp. Na pia meno yangu msidhani ni ya kichaga au Singida au machalii, hapana. Sivuti sigara wala sinywi kahawa.

2. Napenda niwe na ufizi mweusi. Huwa nikimcheck mother akicheka napenda aendelee kucheka. Amebarikiwa kuwa na ufizi mweusi unamtoa sana. Nami nawezaje pata ufizi wa namna hiyo? Je kuna dawa?

Hayo mawili nikiyapata basi ntakuwa nimekamilisha mahitaji yangu yote maana mengine yote yametimiwa yamekosekana hayo mawili tu niridhike.

Ushauri mwingine nishapewa sana kuwa nibaki kama nilivyo n.k sijaujali. Wewe nipe ambao unaendana na matakwa yangu sio matakwa yako.

Nashukuru sana.
 
Tafuta hii dawa ni noma sana
download%20(1).jpeg


Sent using my 6x6 bed.
 
changanya majivu, mkaa na mavi ya mbuzi uwe unatumia kama dawa ya meno alimaarufu dawa ya mswaki
🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄
 
Mkaa. Saga mkaa ukiamka unasugua meno kwa mkaa na chumvi kidogo.
Then unasukutua meno yako. Unasukutua na maji, halafu unatumia sasa dawa ya kawaida ya meno. Fanya mara mbili kwa siku. Ndani ya mwezi tu utakuwa unajichekesha hata kama hujachekeshwa ili tu meno yako watu wayaone.
 
meno yako ni sampuli gani..

mafupi,marefu,mapana,membamba ..au ni manene; jumla una meno mangapi?

pia meno yako yamebanana..au yameachana au hata yanakimbizana.!

mangapi yametoboka... na ulishawahi kungoa ama kuziba

na dawa ya mwisho kutumia ni IPI.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom