Dawa ya mke mkorofi

Dawa ya mke mkorofi

Kama wewe ni mkiristo na una mke mkorofi na umechoka naye ila ukifikiria kumwacha unashindwa kwa vile divorce hairuhusiwi katika christian marriage, jaribu kufanya hivi: mwambie kuwa umefikiria na kuamua kubadili dini. usipoteze muda waone wahusika usilimishwe. hatakataa wewe kubadili dini kwa vile ni haki yako. utakapokuwa converted baada ya muda mwambie dini yako inaruhusu kuoa mke wa pili na una uwezo wa kuwatunza wote. bila kupoteza muda tafuta umpendaye na funga ndoa. Huyo mkorofi atakuwa bi mkubwa na bi mdogo ni huyo mpya. Kama Bi mkubwa atastahimili huo ukewenza ukorofi utakuwa umeisha, lakini uwezekano ni kuwa atafungasha na kutokokomea ajuako yeye. utabaki na Bi mdogo ambaye with time we mwambie umetafakari na kuona huna budi kurejea ktkt dini yako ya awali. chukua hatua haraka na rudi kundini hapo utakuwa umeondokana na kelele. technical divorce!!!! mnasemaje hapo wanaJF?

Usingizi mtamu sana. Afadhali huwa tunalala mda mrefu bila kujua ya duniani kwenu!
 
mke mdogo akiwa mkorofi kuliko mke mkubwa utafanyaje? wewe naee!
ushauri mzuri sana huo hasa kwa akina mama wababe,fasta unabadilisha dini then unaoa halafu yeye anakuwa mke wa pili,du!!! lazima asepe akitimua una rudi kwenye dini yako fasta ha ha ha ha ha ha!!!!!!!!! SAFI SANA
 
Wewe kama yamekushinda usidanganye watu, na ufikirie kama ni kweli unaogopa dini, itakufata tu, sababu sio mkeo anaekataa usioe mke wa pili ni dini, kwa hiyo ukidanganya unakuwa umejidanganya mwenyewe tu
 
kaka, hapo unakuwa umeingia choo cha kike! Kubadili dini tu tayari umesha TRIGGER bomu na ndugu+society. achilia mbali bomu la pili la KURUDI KUNDINI, Albadiri yako!

Mke mkorofi dawa yake ni kuishi nae kwa namna alivyo sababu watu hawana tabia zinazofanana. Cha maana ukorofi wa mkeo usiharibu watoto!!!! Na nina uhakika na ukorofi wote, watoto watakuwa na adabu tu.

Ishi nae kwa shida na raha, amen!
 
Inanikumbusha story moja ambapo, Mume alimuonea wivu Mke wake akidhani, house wife huwa hawana kazi. Hivyo akamwomba Mungu ambadilishe awe mwanamke kwa siku moja tu, ili Mke wake nae aende ofisini aone wanaume wanavyofanya kazi ngumu. Mungu mwenye wingi wa REHEMA akamsikia na akambadilisha akawa Mwanamke... Baada ya kumaliza kazi zote na kuandaa nguo za Mzee na Uniform za watoto kwa ajili ya kesho yake, ilikuwa saa 5 usk. Akapanda kitandani akalala na Mumewe...

Kesho yake akasema. No... Kumbe wanawake wanafanya kazi nyingi sana bora nimuombe Mungu, nirudie kuwa mwanamme.. MUNGU akamwambie, SORRY.. Inabidi usubiri miezi tisa kwanza....
Hahahahahaaaahatwetweeee!!!!!!!? Kwa hiyo mke akaendelea na majukumu yote hata yale ya usiku?
 
hii wala sio technical devorce.......sana nsa utaishi kuoa wake kzaidi na zaid kama mtu ataamua kutumia mbinu yako hii
 
OMG! mkewe alikuwa amempania sana it seems!?:mimba::A S 103:😛ound:
Inanikumbusha story moja ambapo, Mume alimuonea wivu Mke wake akidhani, house wife huwa hawana kazi. Hivyo akamwomba Mungu ambadilishe awe mwanamke kwa siku moja tu, ili Mke wake nae aende ofisini aone wanaume wanavyofanya kazi ngumu. Mungu mwenye wingi wa REHEMA akamsikia na akambadilisha akawa Mwanamke... Baada ya kumaliza kazi zote na kuandaa nguo za Mzee na Uniform za watoto kwa ajili ya kesho yake, ilikuwa saa 5 usk. Akapanda kitandani akalala na Mumewe...

Kesho yake akasema. No... Kumbe wanawake wanafanya kazi nyingi sana bora nimuombe Mungu, nirudie kuwa mwanamme.. MUNGU akamwambie, SORRY.. Inabidi usubiri miezi tisa kwanza....
 
Solution yake ni ngumu sana kuliko tatizo. Ni sawa na ukiulizwa 2+2 = ? Unajibu, 2+2 = 3176 x 6765- 21485638

Basically, the solution is extra extra harder than the problem.
 
Yani huko ndo utakutana na matatizo makubwa bora umvumilie huyo bi mkubwa kuliko kwenda kuoa mke mwingine na itakucost mno make percent kubwa ma bi mdogo hawataki shida na utashangaa ukishamuoa anakuambia anataka nyumba kama aliyonayo bi mkumbwa mara nataka gari kama mke mwenzagu aliyonayo sa hapo kama huna hela ndo utaaendelea kuchanganyikiwa sijui utaenda kuoa mke wa tatu au la!

Ajabu!

Kuna mwenzake mmoja alifanya mchezo kama huo, mwanzoni tulidhani amerogwa ila baada ya kusoma post yako nashawishika kuamini kwamba na yeye aliamua kufanya hivyo akijiona ni mjanja sana. Ni kweli alibadili dini na kuoa mke wa pili kwa ya kiislamu, mke mkubwa akaona ya nini malumbano akaishia zake.

Bi mdogo hakutaka kufanya mchezo fasta akafyatua watoto watatu mfululizo ile mwaka mimba mwaka mtoto, ukichanganya bi mkubwa alikua na mtoto mmoja basi wakawa wanne. Bi mdogo akaanza ukorofi na ni mkorofi kweli kweli mara tatu ya bimkubwa. Bwana anajuta anatamani bora angebaki na bi mkubwa.

Haya sasa hawezi kumuacha huyo akaoa mke wa tatu, kwani nae atataka kuzaa wakati watoto alionao tayari wanamtoa jasho, bi mkubwa aliamua bora mtoto wampleke boarding wasibanane matokeo yake bimdogo anataka na wale watoto wengine wote walipiwe ada kama anayomlipia mtoto wa bimkubwa, baba uwezo huo hana kabaki mwenye mawazo kila kukicha kwani kila kitu bimdogo ni mkorofi. Anatamani bora arudiane na bi mkubwa lakini bimkubwa hataki hata kumsikia, nani anataka kulea mitoto ya mtu tena mitoto imekukuta. Bora hata uliowakuta kwani unakua unajua kabisa mtarajiwa ana mtoto/watoto.

Angalizo:
Ukiona mke ana matatizo jaribu kumrekebisha kwa kumpa viadhabu vya hapa na pale hata kumrudisha kwao akajifunze kama inawezekana. Baada ya jitihada kubwa ikishindikana ndio uamue kuoa mke mwingine ila inabidi uwe makini sana na usikurupuke chukua muda mrefu kama wa mbu, au ukae tu bila mke ulee watoto wako

Ni maoni tu
 
Wewe unapropose kumpiga Mungu chenga unayoita divorce technical.

Mungu hapigiki chenga na wanadamu viumbe wake.
 
Kama wewe ni mkiristo na una mke mkorofi na umechoka naye ila ukifikiria kumwacha unashindwa kwa vile divorce hairuhusiwi katika christian marriage, jaribu kufanya hivi:

Mwambie kuwa umefikiria na kuamua kubadili dini, usipoteze muda waone wahusika usilimishwe. Hatakataa wewe kubadili dini kwa vile ni haki yako. Utakapokuwa converted baada ya muda mwambie dini yako inaruhusu kuoa mke wa pili na una uwezo wa kuwatunza wote.

Bila kupoteza muda tafuta umpendaye na funga ndoa, huyo mkorofi atakuwa bi mkubwa na bi mdogo ni huyo mpya. Kama Bi mkubwa atastahimili huo ukewenza ukorofi utakuwa umeisha.

Lakini uwezekano ni kuwa atafungasha na kutokokomea ajuako yeye, utabaki na Bi mdogo ambaye with time we mwambie umetafakari na kuona huna budi kurejea ktkt dini yako ya awali.

Chukua hatua haraka na rudi kundini hapo utakuwa umeondokana na kelele, technical divorce.

Mnasemaje hapo wanaJF?

Now that is some advice Christians shouldn't follow... Dini ni kitu cha kuchukua makini, mtu anapaswa kuingia dini pya kwa sababu ana imani mungu/miungu wa/ya dini ile ile, na sio kwa sababu anataka kujikwamua mke wake au kupata wake zaidi. Mkristo wa kweli aliye mcha Mungu hatabadilisha dini yake just like that, whenever it's convinient.

On a side note, talaka yaruhusiwa ukristoni ikiwa mmojawapo wa wachumba ametenda kosa la uzinzi.
 
Kacheze kidali po wewe, naona ndoa yako iko kama zile za BABA na MWANA wakati tuko watoto....
 
Back
Top Bottom