Gordian Anduru
JF-Expert Member
- Apr 16, 2021
- 369
- 747
Kulikuwa na mkulima wa matikiti ambaye alisumbuliwa sana na watoto waliokuwa wakivizia na kuiba matiikiti yake.
Siku moja akapata wazo zuri la kuwatisha wale watoto wasimuibie, aliandika bango na kuliweka pale shambani liliilosomeka, “ONYO! Katika haya matikiti kuna moja limechomwa sindano ya sumu” watoto walipofika hawakujua ni tikiti lipi haswa lenye sumu hivyo wakashindwa kuiba lakini hata hivyo na wao wakaamua kufanya jambo la kulipa kisasi.
Mkulima aliipofika shambani kwake siku iliyofuata akakuta bango lingine pembeni ya lile la kwanza linasomeka “Sasa matikiti yaliyochomwa sindano ya sumu yako mawili!”