Dawa ya mtu aliyeungua na maji ya moto

Dawa ya mtu aliyeungua na maji ya moto

nsalu

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
1,189
Reaction score
1,240
Ndugu zangu naulizia dawa ya vidonda vya mtu aliyeungua na maji ya moto.

Ndugu yangu ameungua anatumia dawa ya kupaka inaitwa Silverex ila analalamika maumivu bado ni makali.

Halafu ana kisukari pia.

Naombeni msaada wenu.
 
Pole nyingi kwa mgonjwa!!! Unafahamu dawa ya macho ya mafuta ("achana na ile ya drops inayotibu sikio na macho") tafuta ukipata nimesahau jina lake, Mdogo wangu aliungua tukamwekea hiyo within two weeks ilikuwa iujiza alitembea tulijua atakuwa kilema KBS. Siku nyingine wewe au MTU mwingne akiungua tumia mafuta ya taa km first aid pole sana, MPE na mgonjwa pole nying,majeraha ya kuungua yanauma sana jamani.
 
Asante sana Nosimo na Cham Bee Mungu awabariki
 
Pole! Nenda hospitali usitafute tiba za nyumbani ambazo mara nyingi huleta comlications na vifo. Ufikapo hospitali wataalamu watajua kiasi alichoungua (degree of burn), na kutoa huduma stahili [dawa stahiki za kupaka/kumeza/kuchoma(im/iv) kwa ajili ya kuzuia secondary bacterial infections (local and systemic)].
 
Mtu anatafuta tiba ya haraka we unatuwekea matangazo ya biashara!

Hilo tangazo ndiyo hiyo tiba yenyewe ya haraka.

Kwa mtu aliyeunguwa hakuna tiba ya haraka niliyoiona zaidi ya hiyo kwa sasa. Atumie.

Hilo tangazo linaonesha ni wapi ataipata kwa haraka.

Ninakuomba rudia tena kunisoma.
 
Habari

Mgonjwa wako alitumia dawa ipi? Nina mgonjwa ambaye ni mtoto wangu kaungua maji ya moto ni siku ya tano sasa, unaweza kunisaidia alichoponea mjomba wako?
 
Pole! Nenda hospitali usitafute tiba za nyumbani ambazo mara nyingi huleta comlications na vifo. Ufikapo hospitali wataalamu watajua kiasi alichoungua (degree of burn), na kutoa huduma stahili [dawa stahiki za kupaka/kumeza/kuchoma(im/iv) kwa ajili ya kuzuia secondary bacterial infections (local and systemic)].
Msaada wa haraka please!!!

Kabinti changu kameungua maji ya moto kapo hospital ya mkoa wa morogoro, dawa ipi naweza tumia
 
Tafuta spray inaitwa deep heat itamsaidia na ngozi itakuwa normal
 
Tafuta spray inaitwa deep heat itamsaidia na ngozi itakuwa normal
Japo siku ni nyingi lakini huu ni ukichaa! Wewe,unawatafutia wenzio matatizo! Ile spray uipake kwenye kidonda? Ile kumbuka ni ganzi tu,si kwamba inatibu hivo.
 
Hii mada nimeiona leo,lakini kwa yeyote ambae hakupata jibu, kuna vitu vitatu navyojua viko vizuri sana kwenye majeraha ya kuungua:

1. Aloe vera (mmea huu hupatikana sehemu mbali mbali,na ukibahatisha ule wa asili,kichakani,ni kiboko)

2. Kuna dawa ya meno ya kampuni iliyokuwa inajihusisha na uuzaji wa bidhaa za aloe vera. Hii hata kama ni kidoda kipya umejikata, inakausha haraka sana. Usipoogopa gharama, ni dawa nzuri sana.

3. Asali. Ikiwa haijapitia kiwandani na kuongezewa vikolombwezo vingine,huwa ni nzuri sana
 
Back
Top Bottom