Dawa ya NYONGO au Heartburn

Kule kwetu ikikupata hii tunakunywa magadi. Yale ya kutengeneza kiburu. Kwa huku naona wengine wanakulaga majivu. Mimi nikinywa maziwa fresh huwa namaliza kabisa. Au labda kwa kuwa cha kwangu kinasababishwa na mitungi.

kutengeneza kiburu
yani mkuu umenikuna kweli nimekimis sana sijui lini nitakwenda kwetu
 
kutengeneza kiburu
yani mkuu umenikuna kweli nimekimis sana sijui lini nitakwenda kwetu
Mkuu,
Kiburu hakipiki mijini kwani hakuna vyungu wala magadi yale maalumu kwa Kiburu.
Sijui sana lakini.
 
Punguza kula vichachu, vikali kama vile pilipili, maharage na vyakula vinavyosababisha gesi tumboni. Tafuta dawa za kupunguza heartburn kama vila magnesium - ukipita hata Chemist watakusaidia. Usumbufu ukizidi, muone Dr. usije ukawa unalea vidonda vya tumbo (ulcers).
 
Chris,
Huyu mwenye tatizo hili hata akitumia maziwa au magadi, hapati suluhisho la kudumu.

Tatizo la kiungulia linatokana na Mwili kupungukiwa maji kwa kiasi kikubwa. Ukienda Hospitalini unapewa ant acid kama vile Magnesium trisilicate. Dawa Hizi usaidia kwa muda. Ila tangu sasa ujue kuwa unatakiwa unywe maji ya kutosha. Mwili wako asilimia 72 -75% ya uzito ni maji. Damu ya mwanadamu maji ni asilimia 83%. Ukinywa maji mara kwa mara kwa uchache lita 3 -4 kwa siku ( saa 24) Kiungulia itakuwa hadhithi. Maji (H20) pure water hususan Natural spring Water hayana mbadala. Asikudanganye mtu eti nakunywa bia au soda, vinywaji hivyo hushindandana na mwili na huishia kuchukua maji mwilini, na hivyo vinywaji hivyo vinaponywewa inashauriwa mtu anywe maji kiasi cha ujazo wa bia au soda uliyokunywa. Good luck
 

u are right nlikuwa nasumbuliwa sana na kiungulia after beer, nikaanzisha utaratibu kuwa nilkienda pombeni narudi na lita si chini ya tatu za maji na nayanywa yote kabla ya kulala, tatizo likawa kwishni kabisa, hope to my budy also!
 
ninatatizo hilo, lakini daktari juzi tu kanipa madawa fulani sikumbuki jina, natumia kwa siku 14, kisha amenambia, nikiwa nakunywa bia ama soda lazima ninywe na maji katika uwiano wa moja kwa moja yaani 1:1, hilo ndo suluhisho, sasa na siku ya saba natumia dawa hizo ....ila asanteni kwa useful posts.
 
The Following 3 Users Say Thank You to Exaud J. Makyao For This Useful Post: Emma M. (6th December 2009), Idda (8th December 2009), Omega.Omega (13th December 2009)

kuna hawa watu watatu hata kama post imesema 'sawa mkuu' mnatoa thanks au hamuelewei maana ya thanks? huku ni kupotosha statistics kwa kampeni yenu hiyo chafu!
 
Nashukuru kwa reference mkuu.


Mkuu Exaud, nime-visit hiyo thread ya Sita Sita nikafurahi kuona nondo zilizotolewa humo. Hao wachangiaji makini wako wapi siku hizi? Nadhani wakati huo JF used to be the real home of Great Thinkers!
 
Salaam.
Nisaidie kufahamu 1)kazi ya nyongo kwenye mwili wa binadamu ni nini?
2)Mtu akitapika nyongo kuna umuhimu/faida ipi?(yaani leo kwa mara ya kwanza nimetapika nyongo,sasa nimejikuta nina shauku ya kujua )
 
kazi ya nyongo mwilini ni kusaidia mmeng'enyo wa vyakula vya mafuta, ni njia moja wapo ya kutoa cholesterol mwln, kukipa kinyesi rangi pamoja na nyngnezo.

Kutapika nyongo inaashiria umetapika mda mrefu au mara nyng na umetapika tumbo likiwa halina kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…