Uchovu si Ugomnjwa bali dalili kuwa kuna kitu hakipo sawa katika mfumo wako wa mwili au kimaisha.
Kwa maelezo yako ya awali kuna mambo mawili, Kwanza inaonekana hupati muda wa kupumzika kwa kuchelewa kulala. Kwa mtu mzima huhitaji 8 Hrs kwa mapunziko. Ni wazi kbaisa kuwa kama hupati muda huo, usingizi unakuwa ''cummulative'' na kusababisha ujisikie mchovu.
Pili, muda unaoshinda kwenye computer nao inaweza kuwa sababu, mwanga wa computer, umbali kutoka katika monitor, position ya keyboard na kiti chako vinaweza kuwa ni sababu pia. Watu wengi wanafanya makosa ya kutofanya mazoezi hasa wanapokaa katika hizo computer kwa muda mrefu. Hakikisha kuwa kila baada ya saa moja au na nusu una ''bend & strech'' ili kuweka mwili sawa.
Uchovu pia unaweza kuwa dalili ya maradhi kama ya moyo, kisukari, figo n.k, kwahiyo uwe una check mara kwa mara vitu kama Blood glucose level, Urinalysis, Heart. Kwa uzito wa KG 105 kwa Mississipi U.S.A huo ni uzito wa kawaida tu wa teenager, lakini kwa maumbile yetu Watanzania si wengi wanaofikia hapo, ingawa pia sijui umbile lako halisi. Mazoezi kurudisha uzito nyuma kidogo ningeshauri.
Nashauri usitumie dawa za kupunguza maumivu kama wengi wanavyofanya kwani unaweza kuwa tegemezi wa hizo dawa na ukawa umejenga tatizo lingine. Angalia utaratibu wako wa maisha kwa ujumla kama nilivyoshauri. Namaliza uchovu si ugonjwa bali dalili kuwa kuna something is wrong ima kimwili[ Physical/organic functions] au kimfumo wa maisha ( Sleeping pattern, Occupation, Leisure etc etc)