Mbali ya madikteta wa Afrika walioleta maendeleo ya nchi zao kama Col. Gaddafi na viongozi wa Tunisia, tunaweza kuangalia mifano nje ya Afrika hususan nchi za Asia. Ambapo utawala wa kidikteta umechangia kufanya mapinduzi ya kiuchumi ktk nchi hizo za Asia, na ukiangali wengi wao walitawala vipindi virefu (muda wao wa utawala ktk mabano hapo chini) na wengine alipokea madaraka toka kwa baba zao:
Lee Kuan Yew wa Singapore (1959-1990)
General Park Chung Hee wa South Korea ( 1961-1979)
Chiang Ching Kuo wa Taiwan (1972-1988)
General Suharto wa Indonesia (1967-1998)
Mahathir bin Mohamad wa Malaysia (1981-2003)
Hivyo dikteta akiwa na visheni ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi, historia inaonyesha kuwa kuna matokeo mazuri. Kwanza hakuna muda wa blah blah za kisiasa, matumizi ya kifedha ktk sehemu ya taasisi za kidemokrasia yanakuwa hakuna .e.g hakuna bunge, hakuna wabunge, hakuna vyama vya siasa, hakuna ruzuku kwa vyama, hakuna vyeo vya ukuu wa wilaya n.k Pesa zote zinzooklewa kwa kwa ajili ya kukuza uchumi, miundo mbinu, viwanda n.k