Dada Noella,
Yaani umbile kama lako watu wengi wanahangaika kulipata hata wanalazimika kutokula wakati wana kila kitu. Ningekushauri uridhike na ulivyo kwani baadaye kama wewe ni mweusi utataka uwe mweupe na kama ni mweupe utataka uwe mweusi kitu ambocho baadaye utaonekana kituko.
Asante my dear kwa ushauri.
huwa najisikia vibaya pale napokutana na watu halafu wananambia kuwa unazidi kuwa mdogo tu au hukui..yani mwili wangu ukiniona huwezi kujua nina mtoto, ndiyo maana sipendi nataka ninenepe japo kidogo tu
nikipata mtu kama wewe naoa hapo hapo na ndoa kabisakusema ukweli sikuwa na tatizo hapo mwanzo..ila baada ya kupata mtoto nikajua nitanenepa ila ikawa vice versa mtoto aliacha kunyonya ana miezi tano..nikarudi kwenye kilo zangu na size ile ile ya mwanzo tena naona nimekuwa mdogo zaidi..maneno ya watu ndo yananikosesha raha..eti hukuii,unazidi kuwa mdogoo..aa sasa mi nakosa raha mnoo. Mume wangu nae asubuhi hii ananambia, loo nawe mdogo sana..ndo kisa cha mimi kutaka kunenepa
Salamu wote wanaJF
Mimi ni mama wa mtoto mmoja,nina tatizo la umbile langu yani ni mwembamba ninavaa size 8.kwa kweli huwa nikijiangalia hata sipendezewi na umbo langu,nimekuwa nikila ovyo ili ninenepe lakini wapi..nimekula mpaka cerelac na uji vya mtoto lakini wapi.
sasa nimesikia kuna dawa za kuongeza unene.nahitaji ushauri wenu kwa hili tafadhali.
kuna yeyote aliyewahi kunywa hizo dawa,je zina side effects gani?
au kama kuna njia mbadala naomba ushauri.hata nikivaa nguo sipendezi.
ni kweli dada yangu yaani wenzako wengi wanatafuta miili kama yako,hawali kutwa nzima , sema basi tu umeshaolewa ila nisingekuacha . hauna hata mdogo wako huko/?Asanteni wapendwa kwa kunipa moyo nahisi confidence ilinitoka pale partner wangu alivyonambia hivyo
ila kwa kupata maoni na ushauri wenu nimejisikia mwenye furaha na amani kabisa
@Ivuga..asante, nadhani niliyenae kwa asubuhi ya leo tu hajanipenda gafla jinsi nilivyo ila naona umenena ukweli mtupu
nashukuruni sana
ni kweli dada yangu yaani wenzake wengi wanatafuta miili kama yako,hawali kutwa nzima , sema basi tu umeshaolewa ila nisingekuacha . hauna hata mdogo wake huko/?
Lo, wewe dada una nini, angalia usijaribu dawa utakuja kujuta hata kuzaliwa, mbona wenzio wanahaha kuwa kama wewe wanashindwa, kama ni huyu mumeo anakuambia anapenda unene anakudanganya na si zaidi hata yeye anakuonea wivu na kafugure kako.
Kinachofanya ukonde sana ni hayo mawazo ya kutaka unene, relax kubali ulivyo then the body will come. Yaan km vle una hamu ya kushika mimba ukiiwaza sana haiji ng'oooooo... ukiwa uitaki au ukijiachia na wala hauna shauku nayo ndo inakuja, so u just relax ma dear.
Wenzako tunashinda gym kutafuta kuvaaa size 8, we watafuta dawa ya kufmuka? dahh! Kupendeza kitu gan? Kuwa na akili na roho nzuri then ukiongea mbele za watu utaonekana umependeza tu na utapewa kiti cha mbele, lakini kupendeza kimavazi/ outfit, mmh, huko si kupendeza.
Takatisha na pendezesha ubongo wako na roho yako, huo ndo urembo kamili.