3D.
JF-Expert Member
- Sep 7, 2010
- 1,018
- 284
Pamoja na wadau kusema wembamba sana (size 8) ni sawa tu na kuwa tukubali tu jinsi tulivyo ama wembamba ni urembo, mambo sivyo yalivyo. Binadamu kisaikolojia huwa na wakati anakuwa na udadisi juu ya jinsi watu wanavyomchukulia kimwonekano, kijamii, kifedha (angalau kwa baadhi ya nilivyotaja) n.k. Hiyo ndiyo saikolojia ya kila binadamu. Na jamii imetengeneza "urembo" na "kupendeza" kwa namna "ilivyovumishwa" hadi ikakubalika. Ni kweli kuwa majini (with some exception)/mashetani/mapepo/wachawi hudhaniwa kuwa na sura mbaya (sura mbaya ni ipi?). Waweza kukandamiza uso wako kutoka mashavuni kuelekea mbele na ukafanikiwa kumtisha mtoto mdogo hadi akalia (sura mbaya!!). Dr Remmy, Jangala na Masudi Ally (kama sijakosea jina) walishiriki katika mashindano ya sura mbaya na inakubalika kuwa wana sura mbaya (vigezo ni vipi?) Nachomaanisha hapa ni kuwa jamii imetengeneza "standards" fulani kuhusu mwonekano.
Hii inamaanisha hata dada yetu aliyeanzisha thread hii anaangukia katika vipimo hivi hivi vilivyowekwa (hata kama viko unfair). Hivyo naamini mtu mwenye umbo la wastani (inavyoaminika ni wastani) hupendeza machoni na ni rahisi kupata nguo zinazomtosha vizuri (nguo nyingi zinazotengezwa huwa na size ya kati).
USHAURI WANGU
Hii inamaanisha hata dada yetu aliyeanzisha thread hii anaangukia katika vipimo hivi hivi vilivyowekwa (hata kama viko unfair). Hivyo naamini mtu mwenye umbo la wastani (inavyoaminika ni wastani) hupendeza machoni na ni rahisi kupata nguo zinazomtosha vizuri (nguo nyingi zinazotengezwa huwa na size ya kati).
USHAURI WANGU
- Naunga mkono ushauri uliotolewa katika post namba 18 ya Mayassa hapo juu
- Jitahidi kupata mavazi unaoendana nayo na kama ukiweza "shonesha" ili upate vipimo vyako. Epuka mavazi yenye mistari inayokwenda chini au yenye kitambaa laini sana. Viatu vyenye visigino virefu humfanya mwembamba aonekane mwembamba sana
- Usitilie maanani "sana" mpango wa kunenepa. Wakati mwingine unene huja kutokana na umri.
- Wembamba sana si mzuri. Hata hivyo bora kuwa mwembamba sana kuliko mnene sana.
- Hata usipoongezeka, jiulize marafiki zako wanaendelea kukupenda? Mumeo? Kazini? Mwanao? Comments zipo tu.
- Wakati mwingine tukubali kutofikia viwango fulani vya jamii kwa kuwa hatujafikia na hatutafikia. Najiuliza walemavu wa macho wanajisikiaje!!! Hawatazami mpira, Masanja mkandamizaji, Jukwaa la wakubwa etc. lakini wanajifunza kukubali ukweli.
- Kitendo cha kujua kompyuta kwa Afrika yetu hii, Kitendo cha kuwa JF memba kinakufanya uwe juu, HIVYO UKO JUU NOELLA (Umezaliwa wakti wa Xmas?)