proton pump
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 6,814
- 10,104
Habari ya majukumu! Nisiwe mchoyo wa fadhila Kwani Mungu ametupa Bure, kama unasumbuliwa na vidonda vya tumbo, na una uhakika ndio vyenyewe kweli, kwa maana si kila ugonjwa tumbo ni vidonda vya tumbo, Kuna minyoo, amoeba na typhoid pia ni hatari. Hasa Amoeba dalili zake ni sawa na vidonda vya tumbo, kama unasumbuliwa na amoeba tumia TINIDAZOLE zipo pharmacy. Pia wadudu wa amoeba na typhoid ni hatari Sana hushambulia hadi ubongo kitu kinachosababisha kuchanganyikiwa, kwa dalili tafadhali njoo inbox apo au hadi nianzishe Uzi mwingine.
Hakikisha umepima hayo magonjwa matatu hapo juu kabla ya kuanza kutumia dawa hii ya vidonda vya tumbo usije ukawa na ugonjwa mwingine.
Chukua kiazi ulaya au mbatata au kiazi cha chipsi, kioshe vizuri kwa maji ya moto, usimenye maganda yake Bali kisage kwa ajili ya kutoa juisi kwa kutumia juicer au Greta Ile ya kukwangua karoti hasa Ile sehemu inasaga hadi kinakua kama uji uji kwa ajili ya kutengeneza juisi weka kwenye kikombe, Kisha tia maji vijiko vitano vya chai, kwa nn vijiko vitano? fanya juisi iwe nzito, kunywa juice Yako kama unaweza kiunywa bila kuchuja ni vizuri zaidi, hizo nyuzi nyuzi zinalainisha choo pia,
Dozi kunywa asubuhi kabla hujala chochote, mchana baada ya kula na usiku wakati wa kulala, kunywa kwa mwezi mmoja, dawa hii Haina masharti wa kemikali, na Haina madhara kiafya.
Usisite kunitumia message kwa maendeleo zaidi. Asante.