Dawa za hospital huwa zinazalishwa kwa raw materials gani??

Michosho

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Posts
662
Reaction score
649
Huwa najiuliza, hzi dawa km panadol, antibiotics zote, syrups n.k huwa zinatengenezwa na chemicals ? Km ni chemicals , raw materials zake huwa wana import toka wapi??

Na km ni raw materials huwa ni miti, je, hyo miti huwa ipo hapa tanzania? Na ni wapi huwa inavunwa kwa ajili ya kuletwa viwandani.??
 
Kuna mimea na miti mingi sana ilifanyiwa utafiti wa kisanyansi hivyo ikapatikana kuwa na dawa ambazo zinaweza kumtibu binadamu pia mchanganyiko wa mimea hufanyika ili kupata ratio ya viini ambavyo vikipimwa vinajulikana kuwa vinaweza vikatibu maradhi flani. hivyo ndo dawa huwa zinapatikana, kuna maeneo kuna mashamba yamelimwa na kupandwa mimea ambayo huwa ni dawa na hivyo kuvunwa na kuanza kuwa processed. kama ulisoma masomo ya science uangalie utafiti unavyo fanywa kwenye Chemistry unaweza ukapata idea ya kitu ambacho huwa kinafanyika. mmea huwa unachukuliwa una kamuliwa yale maji na hupelekwa maabara kuangalia yale maji yanamchanganyiko wa nini kemilaki au virutubisho vya aina gani ndo hapo huwa wanaanzia wana sayansi.
 
Hayo maeneo, yaliyopandwa hiyo mimea ya dawa kwa tanzania hapa yako wapi??kwani hapa tanzania pia tunaviwanda.

Na km processing hufanyika nje, so inamaana huwa tuna import material/chemicals hzo za dawa??
 
Hayo maeneo, yaliyopandwa hiyo mimea ya dawa kwa tanzania hapa yako wapi??kwani hapa tanzania pia tunaviwanda.

Na km processing hufanyika nje, so inamaana huwa tuna import material/chemicals hzo za dawa??
Swali zuri sana kama umewahi kufika Arusha nenda jirani na Arusha airport opposite utakuta kuna shamba la Hospitali ya Celian kuna mimea wanapanda hapo huwa ni ikivunwa basi wanayapeleka kwa ajili ya kutengenezea dawa, nina muda mchache hapa ningekuelekeza maeneo mengi, ila hapa nchini tuna viwanda vya kutengeneza dawa vipo kama vingapi hivi ukibahatika kuwatembelewa watakupa ufafanuzi zaidi kuhusu mimea au chemicali wanakozipata za kutengenezea dawa
 
Natamani urudi uendelee kutupa somo mkuu
 
Natamani urudi uendelee kutupa somo mkuu
Mimi fani yangu haiko huko kwenye hayo mambo ya dawa niko kwingine kabisa ila tafiti zangu huwa nazifanya ili nijue na nielewe kwanini hiki na kipi kinakuwaje, ila reference nzuri kama nlivyokueleza viwanda vyenyewe vina majibu mengi zaidi yangu. ila mimi kwa upeo nilionao ningekuwa Waziri wa Kilimo ningetuma team ya wataalam kwenda kukusanya data zinazohusiana na mimea inayosaidia kutengeneza dawa hivyo ningetenga meneo makubwa kama yalivyo mashamba ya miwa na kuwaomba wawekezaji kuendeleza hayo mashamba kwa ajili ya mimea ya dawa tu, kumbuka mimea mingine inahitaji hali ya hewa flani ambayo hata huku tunayo isitoshe aina ya ardhi, tungekuwa na historia kwa kuwekeza kwa makampuni ya dawa.
 
MKUU, MIMEA HYO WANAYOTUMIA WAGANGA WA KIENYEJ NDYO HYOHYO HUTUMIKA KUPROCESS DAWA KIWANDANI.

NADHANI JBU LINATOSHA.
Asante mkuu!
Sasa hyo miti hupandwa wapi??
Kwani viwanda vingi vya dawa viko mjini na mashamba mjini hakuna....
 
Nashukuru kwa ufafanuzi wako mkuu...
Swali langu ni kuwa,.........
Kuna viwanda pale dar vya dawa, lakini sijawahi kuona shamba pale!!
 
Nashukuru kwa ufafanuzi wako mkuu...
Swali langu ni kuwa,.........
Kuna viwanda pale dar vya dawa, lakini sijawahi kuona shamba pale!!
jibu ni kwamba Dar hamnaga mashamba au uliwahi kukuta shamba hapo jijini, hao watakuwa wana import raw material na kutengeneza hapo
 
Kuna baadhi ya mimea tiba huwa inapandwa kwenye mashamba maalumu, mfano dawa ya mseto ya malaria mimea yake inaitwa artemisim huwa inapatikana kwenye mashamba maalum mkoani Iringa.

Pia baadhi ya mimea tiba imetokana na uoto wa asili, hii ina maana hupatikana katika misitu au vichaka n.k
Pia baadhi ya dawa hutengenezwa kiwandani/maabara za dawa, ili iweze kuitwa dawa na kutumika kitaalamu na kisayansi inapitia hatua Mbali Mbali na ni mchakato mrefu na wenye gharama sana hasa inapokuja ugunduzi wa dawa mpya
 
Asante sana.
Hayo mashama maalumu ni kwa viwanda vyote au kila kiwanda kina shamba lake iringa??
Na hzo zinazotengenezwa maabara na kupitia process nyingi, raw materials huwa wana import??
Na hzo zinazopatikana msituni, ni misitu gani hyo na wanatumia manpower gani hyo kukusanya hzo raw materials?? Hzo za msituni haziishi?? Kwani production ya dawa ni endelevu..... Kutokana na demand pia supply kuwa kubwa kwa case ya Tanzania..
 
Katika uzalishaji wa dawa na ili iweze kuitwa dawa inatakiwa iwe na active ingredients ya dawa husika kutegemeana na tiba inayotarajiwa.
Kwa mfano ili mmea wa muarobaini uweze kutengenezwa kutumika kama dawa ya kutibu ugonjwa kama wa malaria au ugonjwa mwingine in lazima ipatikane active ingredients inayotakiwa katika mmea wa muarobaini, active ingredient inaweza ikapatikana na kuchukuliwa kutoka kwenye sehemu za majani, mizizi n.k katika mmea husika.
Dawa zingine hutengenezwa kutokana na muundo wa hormones/vichocheo kwa kushahabiana na kazi inayodhamiriwa kutenda, mfano baadhi ya dawa za kisukari insulin zinajulikana hutengenezwa kutokana na muundo ulioshabihiana na vichocheo kutoka kwa wanyama kama nguruwe, farasi n.k

Angalau kwa ufupi, natumaini umepata picha
 
Asante sana kwa maelezo yako mkuu ..
Sasa hzo active ingredients huwa zinapatika wapi kwa case ya viwandani??
Kwani dawa zipo za aina nyingi sana...
Sasa km wana mashamba , hyo mimea hupandwa sehemu moja, ili kupa hzo active ingredients tofauti tofauti au inakuwaje ??
 
Kuhusu mashamba ya mimea tiba iringa si kwa ajili ya viwanda vyote bali ni makubaliano ya kibiashara ya kilimo cha mimea tiba baina ya kiwanda husika na wanaolima hayo mazao hususan katika utengenezwaji wa dawa za mseto za malaria zinazojulikana kama ALU n.k. Dawa ya mseto kuna ambazo zinatengenezwa China na huwa China wanalima wenyewe ila pia India wanatengeza dawa hizo pia.
Kuhusu malighafi za dawa ndio huwa imported kutegemeana na dawa husika inayotengenezwa, soko lake, sehemu inapotoka n.k
Kuna misitu na uoto wa asili sehemu kubwa katika maeneo yanayotuzunguka, mfano hata hapo ulipo umezungukwa na mimea tiba pia, kwa Tanzania kuna misitu Tabora, Kilimanjaro, Katavi n.k . pia ndani ya hifadhi za misitu na misitu mbali mbali ya jamii. Mapori unayoyaona Bagamoyo, mkuranga na mengineyo yote yana mimea tiba.
Nguvu kazi inayotumika kukusanya mimea hiyo ni kupitia wakulima maalum wenye elimu za dawa au makampuni, taasisi za tiba za asili kama za muhimbili n.k
Eneo hili la ukusanyaji wa malighafi lina fursa nzuri ya kutengeneza fedha.
Misitu huwa inakwisha kutokana na changamoto za mazingira, mabadiliko ya tabia nchi, ukame, ongezeko la idadi ya watu, majanga kama ukame, moto n.k pia kuongezeka kwa shughuli za binadamu kama kilimo na ufugaji zinachangia sana misitu kuisha au uharibifu wa misitu na hifadhi.
Kutokana na hili la uharibifu wa misitu, utengenezaji wa dawa pia hutumia teknolojia kutengeneza dawa kwa kutumia kemikali na njia nyingine badala ya kutegemeana mimea tiba pekee kuhusiana na demand na supply
 
Asante sana kwa maelezo yaliyonipa mwanga ktk hili.
 
Active ingredient kuna ambazo zinatengenezwa viwandani kwa kutumia teknolojia, katika zama hizi computer inahusika sana katika pharmaceutical chemistry, kuna mifumo ambayo inahusisha medicinal chemistry na machine za kutengeneza dawa kurahisisha na kufanikisha utengenezaji wa dawa zenye viwango vya hali ya juu, kwa mfano unaweza ukanunua dawa kama Antibiotic ya India na ya UK ukakuta zona being tofauti ingawa ni dawa moja, sasa hapa ndio kuna issues za ubora wa dawa zinazohusiana na active ingredient na mengineyo halikadhalika active ingredient nyingine hununuliwa kwa kuwa imported kama nilivyo ainisha.
Upandaji au mazao ya mimea tiba hutegemea na teknolojia za kilimo kama matumizi ya greenhouse uwezo wa taasisi , hali ya hewa ya eneo , aina ya mimea n.k
Mfano ukitaka kupata active ingredients za mchaichai itakulazimu upande michaichai halikadhalika kwa mimea mingine n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…